Hamas yatoa radiamali kwa uchaguzi wa utawala wa Kizayuni
(last modified Thu, 19 Sep 2019 01:24:27 GMT )
Sep 19, 2019 01:24 UTC
  • Hamas yatoa radiamali kwa uchaguzi wa utawala wa Kizayuni

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetangaza kuwa kufanyika uchaguzi wa bunge la Israel hakutaleta mabadiliko yoyote katika mwenendo wa muqawama wa Wapalestina.

Abdullatif al Qanoo Msemaji wa Hamas amebainisha kuwa serikali zote za maghasibu wa Kizayuni zinafanana na kila serikali inayoundwa ya utawala huo ni serikali ghasibu na isiyo na umuhimu kwa wananchi wa Palestina. Al Qanoo amongeza kuwa mapambano ya wananchi wa Palestina yatasambaratisha malengo yote ya kiuadui na kiuhasama ya serikali ijayo ya utawala ghasibu dhidi ya wananchi wa Palestina.  

Chama cha Likud kinachoongozwa na Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni kimeshindwa kupata kura zinazohitajika katika uchaguzi wa bunge wa utawala huo ili kuweza kuunda serikali. Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanywa, chama cha Bluu na Nyeupe kinachoongozwa na Benn Gatz mkuu wa zamani wa vikosi vya majeshi ya utawala wa Kizayuni kimeongoza kwa viti viwili yaani kimepata viti 33 na kukipita chama cha Likud kinachoongozwa na Netanyahu ambacho kimeambulia viti 31 katika uchaguzi wa siku ya Jumanne wa utawala huo. 

Benn Gatz, mkuu wa zamani wa vikosi vya majeshi ya Israel
 

 

Tags