Iraq yatangaza marufuku ya kutembea mjini Baghdad kudhibiti ghasia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i56390-iraq_yatangaza_marufuku_ya_kutembea_mjini_baghdad_kudhibiti_ghasia
Waziri Mkuu wa Iraq, Adil Abdul Mahdi ametangaza marukufu ya kutembea watu na magari katika mji mkuu wa nchi hiyo, Baghdad kuanzia alfajiri ya leo Alkhamisi hadi hapo baadaye.
(last modified 2025-11-07T02:31:33+00:00 )
Oct 03, 2019 07:55 UTC
  • Adil Abdul Mahdi
    Adil Abdul Mahdi

Waziri Mkuu wa Iraq, Adil Abdul Mahdi ametangaza marukufu ya kutembea watu na magari katika mji mkuu wa nchi hiyo, Baghdad kuanzia alfajiri ya leo Alkhamisi hadi hapo baadaye.

Marufuku hiyo imetangazwa kufuatia ghasia na machafuko yaliyoanza Jumanne iliyopita katika mji wa Baghdad na mikoa ya kusini mwa Iraq ambayo yamesababisha vifo vya watu kadhaa.

Askari wa kuzuia ghasia wa Iraq wamelazimika kutumia risasi na gesi ya kutoa machozi kuzuia waandamanaji kuingia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad. Vilevile Waziri wa Ulinzi wa Iraq, Najah Hassan Ali Al-Shammari ameviamuru vikosi vya jeshi la nchi hiyo kuwa katika hali ya tahadhari ya juu kutokana na wimbi kubwa la maandamano yamayoshuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Waandamanaji wa Iraq wanataka kuboreshwa hali ya maisha

Maandamano hayo yanafanyika kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutaka kuboreshwa hali ya maisha na kuandaliwa nafasi za kazi na ajira.