Jihad Islami: Mapambano ndio njia pekee ya kuikomboa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i56453-jihad_islami_mapambano_ndio_njia_pekee_ya_kuikomboa_palestina
Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina amesema: "Mapambano na muqawama ndio njia pekee ya kuikomboa Palestina na Wapalestina ni mhimili mkuu wa mapambano hayo."
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 06, 2019 08:20 UTC
  • Jihad Islami: Mapambano ndio njia pekee ya kuikomboa Palestina

Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina amesema: "Mapambano na muqawama ndio njia pekee ya kuikomboa Palestina na Wapalestina ni mhimili mkuu wa mapambano hayo."

Ziyad Al-Nakhaleh Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina aliyasema hayo Jumamosi katika maadhimisho ya mwaka wa 32 wa kuasisiwa harakati hiyo katika Ukanda wa Ghaza. Amesisitiza kuhusu kendeleza njia ya mashahidi, familia za mashahidi, wafungwa na majeruhi wa vita.

Al Nakhaleh amesema Harakati ya Jihad Islami haiwezi kutenganishwa na taifa kubwa la Palestina na kuongeza kuwa: "Pamoja na kuwepo mzingiro, na vizingiti vya kifedha na kisiasa, lakini Wapalestina wangali wanafungamana na mapambano na sasa mapambano hayo ni fahari kwa mataifa yote ya dunia."

Ziyad Al-Nakhaleh Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina

Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami amesisitiza kuwa, kuomba msaada kutoka kwa makatili na kukubali kudhalilishwa na hao makatili ni mambo ambayo hayawezi kuhitimisha mauaji ya Wapalestina. Amesema kuwa, "Taifa la Palestina linafungamana na mapambano ya kupata haki zake katika ardhi zote za Palestina na Wapalestina wote ni taifa moja lililoungana."