Nov 06, 2019 03:07 UTC
  • Russia: Vikwazo vimegeuka na kuwa wenzo wa kuzibana kisiasa nchi nyingine

Waziri Mkuu wa Russia Dmitry Medvedev, amekosoa vikali mienendo ya Marekani ya kutumia siasa za vikwazo dhidi ya nchi nyingine.

Medvedev aliyasema hayo katika kikao na viongozi wa Umoja wa Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia (ASIAN) mjini Bangkok, mji mkuu wa Thailand na kuongeza kuwa, vikwazo vimegeuka na kuwa wenzo wa mashinikizo ya kisiasa na sababu kuu ya kuibuka vita vya kibiashara kati ya nchi za dunia. Waziri Mkuu wa Russia ameongeza kuwa, siasa hizo za vikwazo bila shaka zitaibua vita vikubwa vya kibiashara duniani.

Kikao cha viongozi wa Asian hukoBangkok, mji mkuu wa Thailand

Amebainisha kwamba hali ya sasa ya uhusiano wa nchi za eneo la Asia na azma yao ya kuanzisha soko huria ambalo halitakuwa na ubaguzi, inasisitizia udharura wa kupanuliwa biashara katika eneo hilo. Dmitry Medvedev amesema kuwa, matokeo yanayotokana na utekelezwaji wa siasa za vikwazo na kufuata mfumo huo, kutaibua pande zinazosisitizia udharura wa uzalishaji wa ndani na vita vikubwa vya kibiashara. Kabla ya hapo pia Waziri Mkuu wa Malaysia, Mahathir Bin Mohamad akihutubia mkutano huo wa viongozi wa Umoja wa Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia (ASIAN), alisema kuwa Rais Donald Trump wa Marekani ni mtu asiyefaa kwa ajili ya kufanya naye mazungumzo ya kibiashara.

Tags