Kamanda mwingine wa Jihad Islami ya Palestina auawa shahidi
(last modified Wed, 13 Nov 2019 11:58:04 GMT )
Nov 13, 2019 11:58 UTC
  • Kamanda mwingine wa Jihad Islami ya Palestina auawa shahidi

Kamanda mwingine wa ngazi za juu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina ameuawa shahidi katika hujuma ya ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa mujibu wa taarifa ya Brigedi za Quds, Tawi la Kijeshi la Jihad Islami, Khalid Mavaz Faraj ambaye alikuwa kamanda wa wapiganaji wa harakati hiyo kati mwa Ghaza ameuawa shahidi katika shambulizi la anga la jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel.

Siku ya Jumanne pia, katika hujuma ya ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza, Wapalestina 11 waliuawa shahidi na miongoni mwao alikuwa  Baha Abu al-Ata kamanda wa Jihad Islami. 

Duru za habari zinaarifu kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma zake dhidi ya Ukanda wa Ghaza ambapo hivi karibuni, Wazayuni wamehujumu eneo la makazi ya raia katika kijiji cha Al Nasr kaskazini mwa Rafah.

Hujuma ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza

Jeshi hilo la utawala ghasibu wa Israel ambao unakalia Quds Tukufu kwa mabavu pia limetekeleza mashambulizi ya anga dhidi ya eneo la Khan Yunis na Al Qarara kusini mwa Ukanda wa Ghaza.

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimetangaza kuwa, kufuatia kuvurumishwa makombora ya makundi ya wanamuqawama na wapigania ukombozi wa Palestina ambayo yamelenga ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, watu 41 wamejeruhiwa.

 

Tags