Ujerumani yaituhumu harakati ya muqawama ya Lebanon
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i57989-ujerumani_yaituhumu_harakati_ya_muqawama_ya_lebanon
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani sambamba na siasa za White House ametoa matamshi yasiyo na msingi wowote dhidi ya Hizbullah na kuituhumu harakati hiyo ya muqawama ya Lebanon kuwa ni ya kigaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 19, 2019 21:39 UTC
  • Ujerumani yaituhumu harakati ya muqawama ya Lebanon

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani sambamba na siasa za White House ametoa matamshi yasiyo na msingi wowote dhidi ya Hizbullah na kuituhumu harakati hiyo ya muqawama ya Lebanon kuwa ni ya kigaidi.

Heiko Maas ametoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Harakati ya Hizbullah ya Lebanon na kuitaja kuwa inajihusisha na vitendo vya kigaidi. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amesema kuwa Hizbullah ni tishio kwa Israel na kudai kuwa  kundi hilo linamiliki silaha nyingi. 

Wapiganaji wa Hizbullah ya Lebanon

Maas amedai kuwa Hizbullah ni wakala wa serikali ya Rais Bashar al Assad wa Syria na kutoa wito wa kukabiliana na harakati hiyo ya muqawama ya Lebanon. Viongozi wa nchi za Magharibi wamekuwa wakiituhumu harakati ya Hizbullah ya Lebanon katika hali ambayo harakati hiyo ya muqawama ya Lebanon inatambulika kama chama halali na rasmi katika muundo wa kisiasa wa nchi hiyo na kilicho na wabunge wengi katika bunge la nchi hiyo. Viongozi wa Lebanon siku zote wanaiunga mkono Hizbullah na kuitaja harakati hiyo kuwa iliyotokana na wananchi na jamii ya Lebanon.