Saudi Arabia: Hatukumshinikiza Imran Khan asishiriki mkutano wa Kuala Lumpur
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i58021-saudi_arabia_hatukumshinikiza_imran_khan_asishiriki_mkutano_wa_kuala_lumpur
Saudi Arabia imetangaza kuwa, madai kwamba, nchi hiyo ilimshinikiza Iimran Khan Waziri Mkuu wa Pakistan asishiriki mkutano wa "Kuala Lumpur 2019" hayana ukweli wowote.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 21, 2019 10:08 UTC
  • Saudi Arabia: Hatukumshinikiza Imran Khan asishiriki mkutano wa Kuala Lumpur

Saudi Arabia imetangaza kuwa, madai kwamba, nchi hiyo ilimshinikiza Iimran Khan Waziri Mkuu wa Pakistan asishiriki mkutano wa "Kuala Lumpur 2019" hayana ukweli wowote.

Taarifa iliyotolewa na ubalozi wa Saudi Arabia mjini Islamabad Pakistan sambamba na kubeza mkutano wa Kuala Lumpur kwa kuuita kuwa, "Mkutano Mdogo wa Viongozii wa Kiislamu" imesisitiza kwamba, Riyadh haikumshinikiza Imaran Khan asishiriki mkutano huo. 

Ubalozi wa Saudi Arabia mjini Islamabad Pakistan umetangaza msimamo huo baada ya kuenea taarifa kwamba, Imran Khan Waziri Mkuu wa Pakistan ambaye aliakhirisha kushiriki mkutano wa Kuala Lumpur 2019 katika dakika za mwisho, alifanya hivyo baada ya kkushinikkizwa na utawala wa Riyadh.

Baadhi ya viongozi wa Kiislamu walioshiriki mkutano wa "Kuala Lumpur 2019"

Aidha akihutubia katika mkutano huo nchini Malaysia, Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki alisema kwa, mashinikizo ya watawala wa Saudi Arabia kwa serikali ya Pakistan ndiyo yaliyomfanya waziri mkuu wa nchi hiyo Imran Khan asihudhurie mkutano wa "Kuala Lumpur 2019".

Rais wa Uturuki amesisitiza kuwa, Riyadh ilitishia kwamba, endapo Imran Khan angeshiriki katika mkutano huo ingeondoa akiba yake ya fedha kwenye Benki Kuu ya Pakistan na vile vile ingewafukuza raia milioni nne wa Pakistan wanaofanya kazi nchini Saudia.

Mkutano wa viongozi wa nchi za Kiislamu wa Kuala Lumpur 2019, ulianza rasmi asubuhi ya siku ya Alkhamisi, kwa kuhudhuriwa na viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, mwenyeji Malaysia, Uturuki na Qatar pamoja na mamia ya shakhsia kadhaa muhimu wa nchi za Kiislamu.