Ismail Hania: Tutasimama kidete kukabiliana na mpango wa 'Muamala wa Karne'
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i58770-ismail_hania_tutasimama_kidete_kukabiliana_na_mpango_wa_'muamala_wa_karne'
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa, taifa la Palestina litasimama kidete kukabiliana na mpango wa Muamala wa Karne na kwamba, katu Wapalestina hawataukubali mpango huu uliojaa njama.
(last modified 2026-08-14T10:24:44+00:00 )
Jan 27, 2020 04:44 UTC
  • Ismail Hania: Tutasimama kidete kukabiliana na mpango wa 'Muamala wa Karne'

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa, taifa la Palestina litasimama kidete kukabiliana na mpango wa Muamala wa Karne na kwamba, katu Wapalestina hawataukubali mpango huu uliojaa njama.

Ismail Hania amesema kuwa, yuko tayari kukutana na viongozi wa Harakati ya Fat'h kwa ajili ya kujadili na kupanga mikakati ya kukabiliana na mpango huo wa Marekani wa Muamala wa Karne.

Kioongozi huyo wa Hamas amesisitiza kuwa: Palestina ni ardhi yetu na kito chenye thamani ambacho haiwezekani kufanyika mazungumzo ya kukiuza au kukinunua. Tunatangaza bayana kupinga njama za mpango wa Muamala wa Karne na tanatambua hilo kuwa ni vita; na ni haramu kurejea nyuma katika vita hivyo.

Ismail Hania ameongeza kuwa, kadhia ya Paalestina ni ya umma wote wa Kiislamu na akasisitiza kwamba, kuna ulazima wa kuweko ushirikiano baina ya makundi ya Kipalestina kwa ajili ya kukabiliana na mpango huo mchafu ulio dhidi ya Wapalestina.

Mpango uliojaa njama uliobuniwa na Marekani na Wazayuni wa Israel uliopewa jina la Muamala wa Karne unatazamiwa kuzinduliwa katika kikao cha kesho Januari 28 kati ya Rais Donald Trump wa Marekani na Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa mpango huo, Quds Tukufu itakabidhiwa kwa utawala wa Kizayuni, wakimbizi wa Kipalestina hawatakuwa tena na haki ya kurejea katika ardhi za mababu zao na Palestina itamiliki tu aradhi zilizosalia huko katika Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan na Ukanda wa Gaza.