Ndege ya kijasusi ya muungano wa Saudia yaangushwa kaskazini mwa Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i58804-ndege_ya_kijasusi_ya_muungano_wa_saudia_yaangushwa_kaskazini_mwa_yemen
Ndege isiyo na rubani ya kijasusi ya muungano vamizi wa Saudia imeangushwa katika oparesheni ya pamoja ya Jeshi la Yemen na Kamati za Wananchi wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 28, 2020 21:57 UTC
  • Ndege ya kijasusi ya muungano wa Saudia yaangushwa kaskazini mwa Yemen

Ndege isiyo na rubani ya kijasusi ya muungano vamizi wa Saudia imeangushwa katika oparesheni ya pamoja ya Jeshi la Yemen na Kamati za Wananchi wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa, Kikosi cha Ulinzi wa Angani cha Jeshi la Yemen kikisaidiana na Kamati za Wananchi kimefanikiwa kutungua ndege hiyo ya kijasusi ya Saudia katika eneo la mpakani la  al-Malahit katika mkoa wa Jizan kusini mwa Saudia. Taarifa zinasema ndege hiyo ya kijasusi iliangushwa kwa kombora Jumanne alasiri.

Wiki mbili zilizopita pia Jeshi la Yemen lilitangaza kutungua ndege ya kijasusuI ya Saudia katika eneo la  Jabal Al-Amud katika mkoa wa Jizan nchini Saudia. 

Ndege ya kijasusi isiyo na rubani ya Saudia Arabia ikiwa imeangushwa nchini Yemen

Tokea muungano wa Saudia uanzishe hujuma dhidi ya Yemen Machi mwaka 2015 hadi sasa, makumi ya ndege za kijasusi za Saudia na waitifaki wake zimeangushwa katika oparesheni za Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi la Yemen kikisaidiana na Kamati za Wananchi.

Saudi Arabia na washirika wake wameshindwa kufikia malengo yao katika vita vya Yemen huku wakisababisha maafa makubwa ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuwaua raia wasio na hatia.