Rais Mahmoud Abbas: Hatutaruhusu mpango mchafu wa Muamala wa Karne utekelezwe
(last modified Thu, 06 Feb 2020 12:15:38 GMT )
Feb 06, 2020 12:15 UTC
  • Rais Mahmoud Abbas: Hatutaruhusu mpango mchafu wa Muamala wa Karne utekelezwe

Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kwa mara nyingine tena ametoa radiamali yake kuhusiana na kuzinduliwa mpango mbaya wa Muamala wa karne na kusisitiza kwamba, taifa la Palestina katu halitaruhusu mpangop huo uliojaa njama utekelezwe.

Rais Mahmoud Abbas amesema hayo mjini Ramallah Palestina na kuzitaka nchi za Kiislamu, Kiarabu na mataifa mengine ya dunia kuungana kwa ajili ya kukabiliana na mpango huo wa Marekani na Israel ambao unakanyaga haki za Wapalestina.

Rais huyo wa Mamlakka ya Ndani ya Palestina amebainisha kuwa, mpango huu kama ilivyokuwa mipango mingine iliyojaa njama dhidi ya Wapalestina nao utafeli na kugonga mwamba.

Aidha Mahmoud Abbas ameeleza kuwa, Quds Tukufu na ardhi za Palestina sio bidhaa ya kuuza kwa hivyo Muamala wa karne hautotekelezwa.

Jumanne ya tarehe 28 Januari, Rais wa Marekani, Donald Trump alizindua mpango wa Muamala wa Karne akiwa pamoja na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu. 

Kwa mujibu wa mpango huo wa Marekani, Quds Tukufu itakabidhiwa kwa utawala wa Kizayuni; wakimbizi wa Kipalestina hawatakuwa na haki tena ya kurejea katika ardhi za mababu zao na Palestina itamiliki tu ardhi zitakazosalia huko katika Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan na Ukanda wa Gaza. 

Malalamiko ya kupinga mpango huo wa kidhalimu yangali yanaendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya dunia hususan katika ulimwengu wa Kiislamu.

Tags