Sheikh Isa Qassim: Uislamu unahujumiwa nchini Bahrain
Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain Sheikh Isa Ahmed Qassim ametahadharisha kuhusu njama zinazofanywa na maadui kwa ajili ya kupotosha na kuhariibu sura safi ya Uislamu na kusema kuwa, dini ya Uislamu inahujumiwa na kushambuliwa nchini Bahrain.
Sheikh Isa Ahmed Qassim amesema kuwa, Uislamu unahujumiwa nchini Bahrain katika itikadii, maadili na mieneno yake kutumia anwani na mbinu nyingi zinazogongana na katika nyanja zote za kifikra na kiutamaduni.
Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain ameongeza kuwa, Wabahraini wote wanapaswa kufanya jitihada kubwa za kuondoa hatari hiyo yenye shabaha ya kuwatenganisha Waislamu na dini yao.
Sheikh Isa Qassim amesisitiza kuwa, ili kuweza kulinda Umma wa Kiislamu mbele ya njama hiyo, kuna udharura wa kulindwa dini hiyo na kuwashinda maadui.
Kwa sasa mwanazuoni huyo mkubwa na kiongozi mkuu wa harakati ya upinzani nchini Bahrain anaishi uhamishoni nje ya nchi baada ya utawala wa Bahrain kumpokonya uraia wake.