UN: Israel inaeneza uongo kuhusu Palestina
Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa ameulaumu utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kueneza uongo dhidi ya Wapalestina.
Shirika la habari la Fars limemnukuu Robert Baer, mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabAVu akisema kuwa, viongozi wa Israel wanaamini kuwa Wapalestina wanatumia vifaa vya ujenzi kwa malengo ya kijeshi wakati ambapo hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha jambo hilo.
Robert Baer ameongeza kuwa, Israel mara zote inafanya njama za kila namna za kufanikisha malengo yake dhidi ya Wapalestina
Wakati huo huo Basem Naim, Mkuu wa Baraza la Uhusiano wa Kimataifa katika Ukanda wa Ghaza amesema kuwa, matamshi ya afisa huyo wa Umoja wa Mataifa yanazidi kufichua uongo wa utawala wa Kizayuni kuhusiana na Palestina.
Amesema, lengo la njama hizo mpya za Wazayuni ni kushadidisha mzingiro wa Ghaza.
Katika upande mwingine, Sami Abu Zuhri, Msemaji wa HAMAS amesema, matamshi hayo ya Robert Baer ni ushahidi mwingine wa kuthibitisha uongo unaoenezwa na viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu Palestina.