Iraq kuendelea kushirikiana na Iran, Syria na Russia kupambana na Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i63049-iraq_kuendelea_kushirikiana_na_iran_syria_na_russia_kupambana_na_daesh
Kamandi ya operesheni za pamoja nchini Iraq imesisitiza kuwa, nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Iran, Syria na Russia katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh yaani ISIS na kubadilishana taarifa.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 27, 2020 04:04 UTC
  • Iraq kuendelea kushirikiana na Iran, Syria na Russia kupambana na Daesh

Kamandi ya operesheni za pamoja nchini Iraq imesisitiza kuwa, nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Iran, Syria na Russia katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh yaani ISIS na kubadilishana taarifa.

Meja Jenerali Tahsini al Khafaji Msemaji wa Komandi ya Opeesheni za Pamoja ya Iraq ameashiria kuendelea shughuli za kituo cha usalama cha pande nne katika Wizara ya Ulinzi ya Iraq kwa ajili ya kupambana na Daesh na kueleza kuwa: kituo hicho kinazijumuisha nchi nne yaani Iraq, Russia, Syria na Iran; na kazi yake ni kutoa taarifa, kuratibu taariba baina ya nchi hizo na kuendeleza mapambano dhidi ya Daesh.  

Meja Jenerali al Khafaji ameongeza kuwa, kituo hicho kina nafasi kuu katika mapambano dhidi ya Daesh kupitia uwasilishaji taarifa hususan zile zinazohusu maeneo ya Syria na Iraq. 

Msemaji wa Komandi ya Opeesheni za Pamoja ya Iraq amekanusha habari kwamba, wanajeshi wa muungano wa kimataifa eti wa kupambana na ugaidi wametumwa huko Iraq na kueleza kuwa, wanajeshi wa Marekani ndani ya muungano huo hadi sasa wameshaondoka katika kambi nane ikiwemo ya al Taji; na kambi hizo sasa ziko mikononi mwa wanajeshi wa Iraq. 

Wanajeshi wa Marekani nchini Iraq  

Al Khafaji amesema, kuondoka katika kambi hizo wanajeshi hao wa Marekani hakuna maana ya kuhamia tena wanajeshi hao katika kambi nyinginezo kama zile al Asad na Harir bali hatua hiyo ni kuondoka kikamilifu wanajeshi hao kulingana na muda ulioainishwa na kwa mujibu wa mapatano na serikali ya Iraq. 

Wananchi na makundi mbalimbali ya Kiiraqi wanataka kuona wanajeshi wa Marekani wanatoka nchini mwao. Tayari bunge la Iraq limepasisha rasimu ya kuondoka wanajeshi wa Marekani nchini Iraq.