Umoja wa Mataifa wataka kukomeshwa vita vya Yemen
-
Stéphane Dujarric
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amepongeza hatua ya kubadilishana matekani baina ya serikali ya Sanaa na ile iliyojiuzulu nchini Yemen na kutoa wito wa kukomeshwa vita nchini humo.
Stéphane Dujarric amesema Antonio Guterres amepongeza makubaliano yaliyofikiwa baina ya pande hizo mbili ya kuachia huru mateka 1081 wa vita.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN amezitaka pande mbili hasimu kushirikiana na mjumbe maalumu wa umoja huo katika masuala ya Yemen, Martin Griffiths kwa ajili ya kuhuisha mwenendo wa kisiasa na kukomesha kabisa vita nchini humo.
Jumapili iliyopita Martin Griffiths alitangaza kuwa pande hasimu nchini Yemen zimekubaliana kuachia huru mateka elfu 81 wa vita na kuongeza kuwa, makubaliano hayo ni ishara ya uwezekano wa kupatikana mafanikio katika meza ya mazungumzo.
Faili la kubadilishana mateka wa vita ni miongoni mwa maudhui muhimu katika mazungumzo baina ya Wayemeni na juhudi za kufikiwa mapatano katika suala hili zimekuwa zikikwama mara kwa mara kutokana na vizingiti vya Saudi Arabia.