Msafara mkubwa wa kijeshi wa Marekani waingia Iraq ukitokea Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i64654-msafara_mkubwa_wa_kijeshi_wa_marekani_waingia_iraq_ukitokea_syria
Msafara wa kijeshi wa askari wa Marekani unaojumuisha makumi ya magari ya deraya na vifaru umeingia ndani ya ardhi ya Iraq ukitokea nchi jirani ya Syria.
(last modified 2026-08-23T05:27:14+00:00 )
Nov 16, 2020 03:46 UTC
  • Msafara mkubwa wa kijeshi wa Marekani waingia Iraq ukitokea Syria

Msafara wa kijeshi wa askari wa Marekani unaojumuisha makumi ya magari ya deraya na vifaru umeingia ndani ya ardhi ya Iraq ukitokea nchi jirani ya Syria.

Shirika rasmi la habari la Syria SANA limetangaza kuwa, msafara mkubwa wa kijeshi wa jeshi la Marekani unaojumuisha magari ya deraya yasiyopungua 50 umevuka mpaka wa Syria na kuingia Iraq kupitia kivuko cha Al Walid. Msafara huo wa jeshi la Marekani umetokea kituo cha jeshi la nchi hiyo kilichoko mkoani Al-Hasaka, kaskazini mashariki mwa Syria.

Msafara wa jeshi la Marekani ukiwa katika ardhi ya Syria

Katika miaka ya karibuni, mara kadhaa misafara ya kijeshi ya Marekani inayojumuisha vifaru na zana zingine za kivita imekuwa ikihamishwa baina ya nchi mbili za Iraq na Syria.

Hata hivyo harakati za karibuni za wanajeshi wa Marekani ndani ya nchi hizo mbili imekuwa na umuhimu maalumu baada ya rais wa nchi hiyo Donald Trump kuchukua hatua hivi karibuni ya kumuuzulu waziri wa ulinzi Mark Esper na kumteua Chris Miller kukaimu nafasi hiyo.../