Hizbullah: Tawala za Kiarabu katika eneo hazijawahi kuwa pamoja na Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i65076-hizbullah_tawala_za_kiarabu_katika_eneo_hazijawahi_kuwa_pamoja_na_palestina
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, tawala za Kiarabu zinazotenda jinai katika Mashariki ya Kati hazijawahi kuwa pamoja na Palestina wala kuunga mkono muqawama.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 08, 2020 08:45 UTC
  • Hizbullah: Tawala za Kiarabu katika eneo hazijawahi kuwa pamoja na Palestina

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, tawala za Kiarabu zinazotenda jinai katika Mashariki ya Kati hazijawahi kuwa pamoja na Palestina wala kuunga mkono muqawama.

Sheikh Naim Qassim amesisitiza leo katika maadhimisho ya Intifadha ya Kwanza ya Palestina kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel kwa miaka kadhaa sasa umeghusubu haki za Wapalestina hata hivyo vizazi vya sasa vimebakisha hai malengo ya Palestina.   

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, kitendo cha kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni kimedhihirisha sura halisi ya tawala za Kiarabu zinazotenda jinai kwa malengo ya Palestina; na kuongeza kuwa muqawama utazidisha uwezo na kuwa kwake tayari huko Lebanon, Palestina na katika eneo ili zima kwa ajili ya kuleta mlingano na kuimarisha uwezo wake dhidi ya uvamizi. Imarati na Bahrain tarehe 15 mwezi Septemba mwaka huu zilisaini mapatano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.  

Intifadha ya Kwanza ya Wapalestina ilianza  tangu mwaka 1987; na kumalizika mwaka 1993 kufuatia kusainiwa makubaliano ya Oslo. Intifadha ya msikiti wa al Aqsa yaani Intifadha ya Pili ya Palestina ilianza Septemba 28 mwaka 2000 na kuendelea hadi mwaka 2005; na Intifadha ya Quds yaani Intifadha ya Tatu ya Palestina pia ilianza tarehe Mosi Oktoba mwaka 2015 na ingali inaendelea hadi sasa. 

Wananchi wa Palestina wakikabiliana na polisi wa Kizayuni katika kutetea Msikiti wa al Aqsa