Hania: Hamas ni nembo ya malengo ya Palestina na kuendelezwa muqawama
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i65188-hania_hamas_ni_nembo_ya_malengo_ya_palestina_na_kuendelezwa_muqawama
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa kuundwa harakati ya Hamas kwa hakika ni kule kule kuendelezwa njia ya wananchi wa Palestina yaani kupambana kwa muda mrefu na kudumishwa muqawama tangu kujiri mapinduzi ya Shahid Izzudin Qassam.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 14, 2020 04:26 UTC
  • Hania: Hamas ni nembo ya malengo ya Palestina na kuendelezwa muqawama

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa kuundwa harakati ya Hamas kwa hakika ni kule kule kuendelezwa njia ya wananchi wa Palestina yaani kupambana kwa muda mrefu na kudumishwa muqawama tangu kujiri mapinduzi ya Shahid Izzudin Qassam.

Akihutubia jana usiku katika kumbukumbu ya kutimia mwaka 33 tangu kuasisiwa harakati hiyo, Ismal Hania ameongeza kuwa: Kuundwa harakati ya Hamas kama yalivyo makundi mengine ya Kipalestina si suala la chama kimoja bali ni kadhia ya taifa zima la Palestina; na hatua hiyo inasisitiza kuwa makundi mbalimbali ya Palestina yameasisiwa kwa ajili ya wananchi wa Palestina na kwa lengo la kuwahudumia. 

Hania ameongeza kuwa Hamas imezaliwa kutokana na nyoyo za jamii na kwa mujibu wa malengo ya Palestina; na imepitisha marhala ya kuwa tayari na kujijenga kuelekea kizazi kitakachopelekea kukombolewa ardhi za Palestina na kuendesha mapambano ya wazi na endelevu ambayo yameifikisha kileleni harakati hiyo ya Kiislamu katika ardhi za Palestina. 

Wanamapambano wa harakati ya Hamas ya Palestina 

Katika hotuba yake hiyo kwa mnasaba wa kutimia miaka 33 tangu kuasisiwa harakati ya Hamas, Ismail Hania amesisitiza kuwa: Hamas imeweza kuendesha mapambano ya aina zote na kupitia mapambano hayo imefanikiwa kuasisi kambi yenye nguvu kwa ajili ya muqawama ambayo leo hii inaiwakilisha Ghaza.