Jihad Islami ya Palestina: Wazayuni wanawaogopa wanamuqawama wa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i65433-jihad_islami_ya_palestina_wazayuni_wanawaogopa_wanamuqawama_wa_palestina
Afisa mwanadamizi wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina amesema hujuma za jeshi la utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza ni ishara ya kuchanganyikiwa wakuu wa utawala huo wa Kizayuni ambao sasa wanaogopa makundi wa wanamuqawama au wanamapambano wa Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 27, 2020 11:57 UTC
  • Jihad Islami ya Palestina: Wazayuni wanawaogopa wanamuqawama wa Palestina

Afisa mwanadamizi wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina amesema hujuma za jeshi la utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza ni ishara ya kuchanganyikiwa wakuu wa utawala huo wa Kizayuni ambao sasa wanaogopa makundi wa wanamuqawama au wanamapambano wa Palestina.

Ahmad al Mudallal amesema hujuma ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza jana Jumamosi ni ishara ya kuchanganyikiwa wakuu wa utawala huo ghasibu.

Amesema kuchanganyikiwa huko kumefika kilele baada ya kuvunjwa Knesset, bunge la utawala haramu wa Israel na hivyo kuibua mgogoro wa kisiasa na kijeshi katika utawala huo.

Bunge la utawala haramu wa Israel Knesset lilivunjwa rasmi usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita ambapo kwa kusambaratika serikali ya muungano, sasa uchaguzi mpya wa Bunge ambao ni wanne katika kipindi cha miaka miwili unapasa kufanyika Machi 23 mwaka ujao wa 2021.

Ndege ya kivita ya Israel ikidondosha mabomu Ghaza

Al-Mudalla amesisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni unajaribu kukwepa mgogoro wa kisiasa kwa kushambulia Ghaza ili kudhoofisha irada ya wanamapmbano wa Palestina. Amesema utawala haramu wa Israel hautafanikiwa katika njama zake hizo za kubadilisha mlingano wa nguvu kwani wanamapambano na wanamuqawama hawataruhusu hilo lifanyike.

Jana asubuhi ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel zilishambulia maeneo kadhaa ya Ukanda wa Ghaza na kuwajeruhi watu wawili na kusababisha hasara kwa nyumba za raia, shule, misikiti na maeneo mengine kadhaa.