Watu 28 wameuliwa katika shambulio la magaidi wa Daesh nchini Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i65498-watu_28_wameuliwa_katika_shambulio_la_magaidi_wa_daesh_nchini_syria
Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, makumi ya raia wa Syria wameuawa na kujeruhiwa katika shambulio la kigaidi lililofanywa nchini humo jana Jumatano.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 31, 2020 04:01 UTC
  • Watu 28 wameuliwa katika shambulio la magaidi wa Daesh nchini Syria

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, makumi ya raia wa Syria wameuawa na kujeruhiwa katika shambulio la kigaidi lililofanywa nchini humo jana Jumatano.

Shirika la habari la Syria, SANA limeripoti kuwa, basi moja la abiria lililokuwa likipita katika barabara ya Deir Zor kuelekea Tadmir katikati mwa Syria lilishambuliwa na magaidi wa kundi la Daesh na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 28 na kujeruhiwa wengine wanane. 

Picha zilizorushwa kutoka eneo la tukio zinaonyesha namna basi hilo la abiria lilivyoteketea kikamilifu. Baadhi ya maeneo ya misituni katikati mwa Syria baadhi ya wakati hukumbwa na mashambulizi ya masalia ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh. 

Magaidi wa Daesh nchini Syria 

Bado kuna masalia ya wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh katika maeneo ya msituni katikati mwa Syria licha ya kundi hilo la kigaidi kusambaratishwa nchini humo. Masalia hayo hutekeleza mashambulizi ya kiholela katika maeneo mbalimbali nchini humo.  

Mgogoro ulianza huko Syria tangu mwaka 2011 kufuatia hujuma kubwa ya makundi mbalimbali ya kigaidi kwa uungaji mkono wa Saudi Arabia, Marekani na nchi kadhaa nyingine kwa ajili ya kubadili mlingano wa kieneo kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni. Jeshi la Syria hivi karibuni lilifanikiwa kufunga faili la kundi la kigaidi la Daesh huko Syria kwa msaada wa washauri wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia.