Maduro; Venezuela imemshinda Trump
(last modified Thu, 21 Jan 2021 11:39:53 GMT )
Jan 21, 2021 11:39 UTC
  • Maduro; Venezuela imemshinda Trump

Rais wa Venezuela amekutaja kuondoka huko White House Rais wa zamani wa Marekani kuwa ushindi kwa nchi yake.

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela ameeleza kuwa nchi yake imeweza kukabiliana na siasa za Rais Donald Trump na hatimaye kumshinda. Rais Maduro alisisitiza jana baada ya kula kiapo Rais mpya wa Marekani Joe Biden kwamba: Leo Januari 20 Donald Trump ameondoka, ameondoka, ameondoka, sisi tumemshinda. Amesema hatua hiyo ni ushindi kwa Venezuela. Rais Maduro ameongeza kuwa,  Trump ameondoka peke yake na huo ni ushindi kwa Venezuela.  

Rais wa Venezuela aidha ametuma ujumbe kwa njia ya televisheni akiinasihi serikali mpya ya Marekani iache kuyatia dosari mapinduzi ya Bolivia na kumchafulia jina Nicolaus Maduro na kuitaka ifunge ukurasa wake wa uwongo, uenezaji fitina na uhasama dhidi ya Venezuela.  

Hii ni katika hali ambayo Antony Blinken Waziri wa Mashauri ya Kigeni aliyependekezwa na rais mpya wa Marekani Joe Biden jana alidhihirisha sera za uhasama za Washington dhidi ya Maduro katika Kongresi ya nchi hiyo na kusisitiza kuwa Washington ingali inamtambua rasmi Juan Guaido aliyejitangaza kuwa Rais wa Venezuela na kinara wa upinzani nchini humo. 

JuanGuaido, kiongozi kibaraka mpinzani wa serikali ya Caracas 

Katika kipindi cha utawala wa Rais Donald Trump Marekani haikusita kuchukua hatua mbalimbali kuanzia vikwazo hadi hatua za kijeshi ili kupindua serikali halali ya Rais Maduro.  

 

Tags