Bunge la Ureno launga mkono 'Mshikamano na Taifa la Palestina'
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i7237-bunge_la_ureno_launga_mkono_'mshikamano_na_taifa_la_palestina'
Bunge la Ureno limepitisha kwa wingi mkubwa wa kura rasimu ya mpango wa kuonesha mshikamano na taifa la Palestina na kulaani ukiukaji wa haki zao za msingi unaofanywa katika ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 17, 2016 03:22 UTC
  • Bunge la Ureno launga mkono 'Mshikamano na Taifa la Palestina'

Bunge la Ureno limepitisha kwa wingi mkubwa wa kura rasimu ya mpango wa kuonesha mshikamano na taifa la Palestina na kulaani ukiukaji wa haki zao za msingi unaofanywa katika ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu.

Bunge la Ureno limeunga mkono rasimu ya mpango wa "Mshikamano na Taifa la Palestina" uliowasilishwa na chama cha mrengo wa kushoto na kusisitiza kuendelezwa jitihada za kuleta amani na mapatano ya kiadilifu katika eneo la Mashariki ya Kati, kuundwa nchi huru ya Palestina na kudhaminiwa matakwa ya haki ya Wapalestina ikiwemo haki ya kuamua juu ya mustakabali wao na kuishi maisha ya heshima.

Mpango huo wa "Mshikamano na Taifa la Palestina" umeashiria kuendelea hali ngumu inayowakabili wakimbizi wa Kipalestina tangu mwaka 1948 hadi sasa na kueleza kwamba idadi ya wakimbizi wa Kipalestina imekadiriwa kupindukia milioni tano ambapo licha ya maazimio ya Umoja wa Mataifa, likiwemo azimio nambari 194, wakimbizi hao hadi sasa wameshindwa kurejea kwenye miji na makazi yao ya asili.

Ni muhimu kuashiria kwamba Jamii ya Kimataifa imeyanyamazia kimya maafa ya kuvamiwa na kukaliwa kwa mabavu Palestina mwaka 1948 katika hali ambayo baada ya kupita miaka 68 tangu kuvamiwa na kukaliwa kwa mabavu ardhi hiyo uangamizaji wa kizazi, uvamizi na jinai za utawala haramu wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina zingali zinaendelea.../