Saudia yaendelea kukiuka usitishaji vita nchini Yemen
Kwa mara nyingine ndege za Saudia zimeendelea kukiuka makubaliano ya usitishaji vita katika maeneo tofauti nchini Yemen.
Ndege za Saudia jana Alkhamisi zilishambulia mikoa ya Sana'a, Taiz, Al Jawf, Ma'rib, Saada, Al Mahwit, Al Hudaydah, Dhale, Hajjah na Omran nchini Yemen. Mashambulizi ya ndege hizo za utawala wa Aal-Saud yamesababisha watu kadhaa kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Wanawake na watoto ni miongoni mwa waathiriwa wa hujuma hizo za kikatili za ndege za Saudi Arabia hapo jana. Muungano wa baadhi ya nchi za Kiarabu unaoongozwa na Saudia chini ya uungaji mkono kamili wa Marekani na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ulianzisha mashambulizi yake mwezi Machi mwaka jana nchini Yemen kwa lengo ya kutaka kumrejesha madarakani kibaraka wake yaani rais wa zamani wa Yemen aliyejiuzulu wadhifa huo na kukimbilia Saudia, Abd Rabbuh Mansur Hadi. Licha ya mashambulizi hayo makubwa kusababisha hasara isiyoelezeka ikiwemo mauaji ya maelfu ya raia wa Yemen hususan wanawake na watoto na kuharibu miundombinu mbalimbali, lakini yameshindwa kabisa kufikia malengo yake.