Marekani yaua watoto, wanawake katika operesheni ya kijeshi Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i79944-marekani_yaua_watoto_wanawake_katika_operesheni_ya_kijeshi_syria
Kwa akali raia 13 wakiwemo watoto saba na wanawake watatu wameuawa katika operesheni ya kijeshi ya Marekani dhidi ya wakazi wa mkoa wa Idlib, kaskazini magharibi mwa Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 03, 2022 09:18 UTC
  • Marekani yaua watoto, wanawake katika operesheni ya kijeshi Syria

Kwa akali raia 13 wakiwemo watoto saba na wanawake watatu wameuawa katika operesheni ya kijeshi ya Marekani dhidi ya wakazi wa mkoa wa Idlib, kaskazini magharibi mwa Syria.

Duru za kiusalama zimeripoti kuwa, raia hao wameuawa katika operesheni iliyofanywa na vikosi maalumu vya jeshi la Marekani katika mkoa huo unaopakana na Uturuki, ambayo ni ngome ya mwisho ya mabaki ya makundi ya kigaidi nchini Syria.

Wakazi wa mji wa Atmeh mkoani hapo wamenukuliwa na shirika la habari la Associated Press wakisema kuwa, maiti za raia zimetapakaa katika eneo hilo kufuatia hujuma hiyo ya usiku wa kuamkia leo ya wanajeshi vamizi wa Marekani.

Wakazi hao wamesema raia wasio na hatia ndio waliolengwa kwenye shambulio hilo, kwani helikopta za Marekani zimedondosha mabomu kwenye majengo yenye makazi ya raia mkoani Idlib.

Wamarekani wakiiba mafuta ya Wasyria

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon), John Kirby amedai kuwa operesheni hiyo imelenga magenge ya kigaidi huko kaskazini magharibi mwa Syria, na eti imefanyika kwa mafanikio makubwa, na kwamba hakuna askari wa US aliyeuawa.

Hii ni katika hali ambayo, Marekani na utawala haramu wa Israel ni waungaji mkono wakubwa wa magaidi ambao wanataka kuiangusha serikali halali ya Rais Bashar al Assad nchini Syria.