Uungaji mkono wa Uturuki kwa utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i82338-uungaji_mkono_wa_uturuki_kwa_utawala_wa_kizayuni
Matukiko yanayoshuhudiwa sasa huko Uturuki kufuatia nchi hiyo kuingilia kijeshi baadhi ya nchi jirani na kujaribu kuyakalia kwa mabavu baadhi ya maeneo ya Syria na Iraq; matatizo ya nchi hiyo katika sekta za kiuchumi, kisiasa na kijeshi hivi sasa yameongezeka pakubwa tangu mwaka 2018.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 09, 2022 23:47 UTC
  • Uungaji mkono wa Uturuki kwa utawala wa Kizayuni

Matukiko yanayoshuhudiwa sasa huko Uturuki kufuatia nchi hiyo kuingilia kijeshi baadhi ya nchi jirani na kujaribu kuyakalia kwa mabavu baadhi ya maeneo ya Syria na Iraq; matatizo ya nchi hiyo katika sekta za kiuchumi, kisiasa na kijeshi hivi sasa yameongezeka pakubwa tangu mwaka 2018.

Baada ya Uturuki kuingilia kijeshi masuala ya Syria na Iraq licha ya serikali za Damascus na Baghdad kupinga suala hilo; serikali ya nchi hiyo chini ya uongozi wa Rais Recep Tayyep Erdogan na akthari ya nchi zenye mfungamano na mrengo wa Magharibi katika eneo la magharibi mwa Asia zimekabiliwa na matatizo mengi. Baadhi ya matatizo hayo ni natija ya uhusiano wa pande mbili za Uturuki na utawala wa kibaguzi wa Israel, Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) na Saudi Arabia pamoja na Bahrain; huku mengine yakiwa yamesababishwa na siasa za serikali ya Erdogan katika eneo. 

Ukweli huu pia haupasi kupuuzwa kwamba, jithada za viongozi wa serikali ya Ankara za kudhihirisha sera zao huru mkabala wa masuala ya kieneo na kimataifa na wakati huo huo kutaka kujiweka mbali na Marekani na Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (Nato) na badala yake kufuata sera za Umoja wa Ulaya, yote hayo yameandaa uwanja wa kuibuka matatizo ya nchi hiyo moja baada ya jingine. Wakati huo huo harakati za  kijeshi za Uturuki mashariki mwa bahari ya Mediterania mbali na uvamizi wake huko Syria na Iraq pia ni kisingizio kingine tosha kinachotumiwa na serikali za Magharibi kukabiliana na matakwa na maslahi ya Uturuki katika bahari hiyo na hata huko Syria. 

Kuibuka kwa mivutano kati ya Uturuki na waitifaki wake wa Magharibi katika eneo kumewazidishia matatizo zaidi viongozi wa serikali ya Ankara; na wakati huohuo kuisabababishia nchi hiyo migogoro ya kiuchumi na kifeha mmoja baada ya mwingine. Viongozi wa Uturuki tangu miezi ya mwishoni mwa mwaka uliopita wa 2021 wamechukua hatua za kubadilisha siasa zao mkabala wa Marekani, Ulaya, utawala wa Kizayuni, Saudia, Imarati na Misri kwa kudhani kuwa matatizo yanayoisibu nchi yao yanatokana na harakati za washirika wa zamani wa nchi hiyo. Mabadilko hayo ya sera za serikali ya Erdogan ambayo yametajwa na duru za kisiasa ndani ya Uturuki kama hatua za ukandamizaji; hadi sasa si tu yameshindwa kupunguza matatizo ya nchi hiyo bali yameshadidisha zaidi hali ya mgogoro nchini humo.

Rais Recep Tayyep Erdogan wa Uturuki 

Bila shaka tunapasa kusema kuwa,  kushtadi mgogoro wa kiuchumi na matatizo ya kifedha pamoja na ughali wa maisha unaowakabili wananchi wa Uturuki; kunaonyesha namna siasa za nje za serikali ya Rais Recep Tayyip Erdogan kwa mara nyingine tena zilivyojikita katika kuanzisha ushirikiano na utawala ghasibu wa Israell unaoikalia Quds Tukufu kwa mabavu, Marekani, Misri na serikali za Kiarabu za eneo la Ghuba ya Uajemi. Hii ni katika hali ambayo, matatizo makuu ya serikali na watu wa Uturuki yameshuhudiwa baada ya nchi hiyo kuzishambulia nchi jirani zake. Hata hivyo inaonekana kuwa, viongozi wa serikali ya Erdogan wanadhani kuwa wataweza kuondokana na matatizo ya ndani na kikanda yanayoikabili nchi hiyo kwa Ankara kuachana na siasa za za kuipinga mirengo ya Magharibi na Uzayuni wa kimataifa. Nchi za kieneo ambazo zina mgongano wa kimaslahi na Uturuki zinatambua ukweli huu kwamba, serikali ya Erdogan inapasa kuafiki ushirikiano huo tajwa ili kuhitimisha mgogoro wa kiuchumi na kifedha pamoja na matatizo ya watu wa nchi hiyo. Kuhusiana na hilo, tovuti ya Davar ambayo ni moja ya duru za habari za mrengo wa kushoto ya lugha ya Kiibrania imemnukuu mchambuzi mmoja wa tovuti hiyo na kuandika: Matatizo ya kiuchumi na kuongezeka pakubwa gharama za maisha na wakati huo huo kuanguka thamani ya sarafu ya Uturuki kumempelekea Erdogan atazame upya mahesabu yake ya kisiasa na kufanya juhudi za kuboresha uhusiano wake na baadhi ya pande za kieneo ikiwemo Israel, Misri na Saudi Arabia." 

Ala kulli hal, baada ya mazungumzo ya karibuni kati ya Erdogan na Rais wa utawala wa Kizayuni, serikali ya Ankara na hasa Rais huyo wa Uturuki alighafilika kuunga mkono malengo ya wananchi wa Palestina. Hilo linaonyesha kuwa viongozi wa Uturuki zaidi wanakimbilia kutoa matamko na nara tupu kuliko kuchukua hatua kivitendo. Kwa ibara nyingine ni kuwa, serikali  ya Rais Erdogan ambayo siku zote imekuwa ikiunga mkono malengo ya wananchi wa Palestina kupitia nara na matamshi yake hivi sasa imedhihirisha mtazamo dhidi ya serikali na wananchi wa Palestina. Katika radiamali yake ya kwanza kabisa kufuatia oparesheni ya kujitolea kufa shahidi iliyotekelezwa Alhamisi usiku na mwanamuqawama wa Hamas huko Israel, Rais wa Uuturuki amelaani oparesheni hiyo. Ubalozi wa Uturuki katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu umeuunga mkono utawala wa Kizayuni na kulaani oparesheni hiyo ya kujitolea kufa shahidi huko Tel Aviv na kusema unatiwa wasiwasi na kuongezeka oparesheni kama hizo.  Wakati huohuo ubalozi huo pia umetoa taarifa na kutoa mkono wa pole kwa familia za wahanga wa Kizayuni. Akijibu msimamo huo wa serikali ya Uturuki, Hazim Qassim Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ametoa radiamali hasi kwa msimamo huo wa Uturuki mkabala wa oparesheni hiyo ya kujitolea kufa shahidi iliyotekelezwa na kijana wa Kipalestina huko Tel Aviv. Hazim Qassim amesema: Hamas inalaani msimamo wa Uturuki wa kulaani oparesheni ya kujitolea kufa shahidi dhidi ya maghasibu wa Kizayuni. "  

Hazim Qassim, Msemaji wa harakati ya Hamas ya Palestina 

Kiujumla tunapasa kusema kuwa, tukitazama matatizo iliyonayo Uturuki hivi sasa kama mgogoro wa kiuchumi na matatizo ya kifedha ikiwemo kuanguka kwa sarafu ya nchi hiyo tunaona kuwa, masuala hayo hayana uhusiano wowote na kuanzisha uhusiano na pande kama utawala wa Kizayuni. Bila shaka Uturuki itaendelea kukumbwa na matatizo ya kiuchumi na kifedha madhali inaendelea kuzikalia kwa mabavu ardhi za Syria na Iraq.