Walowezi wa Kizayuni wavamia Msikiti wa Al-Aqsa, Hamas yatoa onyo
Idadi kubwa ya walowezi wa Kizayuni wenye itikadi kali waliuvamia na kuuvunjia heshima Msikiti wa Al-Aqsa mjini Quds (Jerusalem) mapema Jumapili wakati utawala dhalimu wa Israel uikuwa ukiwashaambulia na kuwaua Wapalestina kwa mabomu huko Gaza kwa siku ya tatu mfululizo.
Wakilindwa na askari katili wa Israel waliokuwa wamejizatiti kwa silaha nzito nzito, walowezi wa Kizayuni walianza uvamizi huo mapema Jumapili asubuhi kwa saa za huko na kuendelea kwa saa tatu, katika siku ambayo kulikuwa kunaadhimishwa sikukuu ya Kiyahudi ya Tisha B'av.
Uvamizi hui umeandaliwa na vikundi vya Kizayuni vyenye siasa kali za mrengo wa kulia vinavyotaka kuharibiwa kwa Msikiti wa Al-Aqsa, mojawapo ya maeneo takatifu zaidi katika Uislamu.
Walowezi wa Kizayuni waliinua benera za Israel huku wakitekeleza ibada za Kiyahudi ndani ya uwanja wa Msikiti wa Al Aqsa.
Uvamizi wa Wazayuni dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa siku ya Jumapili uliruhusiwa na mamlaka ya Israel licha ya wasiwasi kwamba hatua hiyo inaweza kuzua ghasia zaidi wakati wa kampeni ya kinyama ya kijeshi ya Israel inayoendelea huko Gaza.
Zaidi ya Wapalestina 31 wakiwemo watoto sita wameuawa katika mashambulizi hayo yaliyoanza siku ya Ijumaa. Takriban 253 walijeruhiwa, zaidi ya nusu yao wakiwa wanawake na watoto, kulingana na wizara ya afya ya Palestina.
Wakati huo huo Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imetoa onyo kali baada ya Wazayuni kuuvamia Msikiti wa Al Aqsa na kutoa wito kwa Wapalestina kukabiliana na uchokozi huo wa Wazayuni ili kulinda ardhi za Palestina na maeneo yake matakatifu.