Mwakilishi wa Wazayuni akiri: Wapalestina wana haki ya kujilinda
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i88366-mwakilishi_wa_wazayuni_akiri_wapalestina_wana_haki_ya_kujilinda
Mwakilishi wa Bunge la utawala wa Kizayuni (Knesset) amekiri kuwa Wapalestina wanaowafyatulia risasi wanajeshi wa utawala huo si magaidi, na kwamba wana haki ya kujilinda kwa mujibu wa sheria za Umoja wa Mataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 20, 2022 03:27 UTC
  • Mwakilishi wa Wazayuni akiri: Wapalestina wana haki ya kujilinda

Mwakilishi wa Bunge la utawala wa Kizayuni (Knesset) amekiri kuwa Wapalestina wanaowafyatulia risasi wanajeshi wa utawala huo si magaidi, na kwamba wana haki ya kujilinda kwa mujibu wa sheria za Umoja wa Mataifa.

Wanajeshi wa Israel na walowezi wa Kizayuni kila uchao huwauwa shahidi, kuwajeruhi na kuwatia nguvuni wananchi madhlumu wa Palestina kwa visingizio mbalimbali. Katika kujibu jinai hizo za Wazayuni, raia wa Palestina pia hutekeleza oparesheni za kimuqawama kuwalenga maghasibu Wazayuni. 

Baadhi ya Wazayuni wanapinga sera za ukandamizaji na za mabavu zinazotekelezwa na jeshi la utawala huo ghasibu licha ya  mrengo wa kulia wenye misimamo mikali wa Kizayuni kutekeleza sheria kali za kijeshi katika mitaa ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kuliruhusu jeshi la utawala huo kuchukua hatua kali za kiusalama ili kuwakandamiza vikali Wapalestina na eti kujibu mashambulizi ya karibuni ya kujitolea mhanga ya raia wa Palestina. 

Ofer Cassif, Mwakilishi katika bunge la utawala wa Israel (Knesset) amesema, kwa mujibu wa tafsiri iliyokubalika katika ngazi ya kimataifa na kama ilivyobainishwa wazi na Umoja wa Mataifa, raia ambao ardhi zao zimeghusubiwa wana haki ya kutumia silaha na kupambana na wavamizi. 

Mbunge wa mrengo wa kulia wa bunge la Israel (Knesset)

Zaidi ya oparesheni za kimuqawama 7,200 zimetekelezwa na Wapalestina dhidi ya Wazayuni tokea mwanzo wa mwaka mwaka huu hadi tarehe 6 mwezi huu wa Septemba.  

Viongozi wa utawala wa Kizayuni wamezidi kuingiwa na wahka na kukumbwa na wasiwasi kufuatia kupamba moto mapambano ya silaha ya makundi ya muqawama ya Palestina khususan katika miji miwili ya Nablus na Jenin ambayo inatambulika kama kitovu cha mapambano katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Hii ni kwa sababu, awali viongozi hao wa Kizayuni walikuwa wakihofa tu muqawama wa Wapalestina huko Ghaza yaani upande wa kusini lakini hivi sasa mapambano katika Ukingo wa Magharibi yamekuwa changamoto kubwa kwa watawala wa Israel; ambapo hali ya kisiasa inayolegalega sasa inashuhudiwa huko katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.