Wanamapambano wa Palestina: Adui hajui isipokuwa lugha ya mabavu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i89850-wanamapambano_wa_palestina_adui_hajui_isipokuwa_lugha_ya_mabavu
Makundi ya muqawama wa Palestina yamepongeza operesheni ya wanamapambano wa Kipalestina katika mji wa al Khalil huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kusisitiza udharura wa kuendelezwa mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni wakisema, utawala huo hauelewi isipokuwa lugha ya mabavu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 30, 2022 04:34 UTC
  • Wanamapambano wa Palestina: Adui hajui isipokuwa lugha ya mabavu

Makundi ya muqawama wa Palestina yamepongeza operesheni ya wanamapambano wa Kipalestina katika mji wa al Khalil huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kusisitiza udharura wa kuendelezwa mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni wakisema, utawala huo hauelewi isipokuwa lugha ya mabavu.

Ni baaa ya operesheni iliyotekelezwa na mpiganaji wa Kipalestina "Mohammed Kamal al-Ja'bari" katika mji wa al Khalil ulioko kusini mwa Ukingo wa Magharibi, ambapo Mzayuni mmoja aliuawa na wengine 5 kujeruhiwa.

Vyombo vya habari vya Kizayuni vimethibitisha kutokea kwa operesheni hiyo na kuripoti kuwa, hali ya majeruhi 2 wa operesheni hiyo ni mbaya.

Tariq Ezzeddin, Msemaji wa Harakati ya Jihad Islami katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan amesisitiza kuwa, operesheni ya al Khalil ilifanywa ili kuueleza utawala ghasibu wa Israel kuwa taifa la Palestina liko huru na litautimua utawala wa Kizayuni katika ardhi yake.

Amesema operesheni hiyo ni jibu kwa uhalifu na jinai zinazofanwa na Israel na inatoa ujumbe kwamba damu ya mashahidi wa Kipalestina wa Ukingo wa Magharibi haitapotea bure na wala mashujaa hao hawatasahaulika.

Ismail Rizwan, mmoja wa viongozi wakuu wa harakati ya Hamas pia ametoa wito wa kuzidishwa mapambano dhidi ya utawala ghasibu na kusisitiza kuwa utawala huo hauelewi chochote isipokuwa lugha ya mabavu.

Kamati ya Muqawama wa Palestina pia imesisitiza kuwa taifa shujaa la Palestina limethibitisha tena kwamba sasa ni wakati wa kuzungumza bunduki na silaha za wapigania uhuru.

Harakati ya Mujahidina wa Palestina pia imewapongeza wapiganaji wa Jihadi wa Palestina kwa operesheni hiyo ya al Khalil na kubainisha kwamba, operesheni hiyo imethibitisha kuwa, mapigano na mapigano na utawala wa Kizayuni ndio njia bora ya kukabiliana na utawala huo kwa sababu Wazayuni hawaelewi chochote isipokuwa lugha ya mabavu.