Jihadul-Islami: Palestina haikubali kugawana ardhi na utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i91988-jihadul_islami_palestina_haikubali_kugawana_ardhi_na_utawala_wa_kizayuni
Mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amesema, taifa la Palestina limethibitisha kwa damu safi ya vizazi vyake kwamba kamwe halitakubali kufanyika mgawanyo kati ya mataifa mawili na nchi mbili.
(last modified 2026-07-31T06:29:55+00:00 )
Dec 22, 2022 04:28 UTC
  • Jihadul-Islami: Palestina haikubali kugawana ardhi na utawala wa Kizayuni

Mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amesema, taifa la Palestina limethibitisha kwa damu safi ya vizazi vyake kwamba kamwe halitakubali kufanyika mgawanyo kati ya mataifa mawili na nchi mbili.

Khalid al-Batsh, ameyasema hayo katika kumbukumbu ya kuuawa shahidi Majid al-Harazin, mmoja wa makamanda wa Brigedi ya Quds, na kubainisha kwamba "njama za kushambulia Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa lengo la kupanua vitongoji vya walowezi na kuishambulia Quds na kuwahamisha kwa nguvu wakazi wake na kulipiza kisasi dhidi ya Lebanon na Gaza yote hayo yanaonyesha kuwa chaguo la kufuata ni kukabiliana na adui kwa vita na hii inatufanya tuendeleze muqawama na mapambano ya silaha dhidi yake".
Khalid al-Batsh

Al-Batsh ameongezea kwa kusema: "jukumu la wapiganaji vita la kukabiliana na wavamizi wa Kizayuni halitasitishwa katu, kwa sababu jukumu letu katika ardhi ya Palestina ni kutomruhusu adui akae humo; na tunaendeleza mapigano ili kufikia kwenye hali mwafaka na ya kuridhisha".

Afisa huyo wa Harakati ya Jihadul-Islami ameashiria pia hatua ya tawala za Kiarabu ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na akayataka mataifa ya Kiarabu kuangalia upya hatua iliyochukuliwa huko nyuma ya kuanzisha uhusiano na adui Mzayuni na kusimamisha mchakato huo wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na adui huyo wa umma.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Khalid al-Batsh ametoa wito wa kuungwa mkono zaidi wapiganaji wa muqawama wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Wapalestina wanaozingirwa huko Gaza na Baitul Muqaddas ili kuimarisha muqawama na kuzitia nguvu zaidi harakati za kurejesha haki za wananchi wa Palestina.../