Saleh: Hujuma dhidi ya Yemen ni uchokozi wa Mawahabi, magaidi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i9997-saleh_hujuma_dhidi_ya_yemen_ni_uchokozi_wa_mawahabi_magaidi
Ali Abdullah Saleh, mkuu wa chama cha Kongresi ya Kitaifa nchini Yemen ambaye pia ni rais wa zamani wa nchi hiyo, amesema kuwa, hujuma za Saudia dhidi ya nchi hiyo ni uchokozi wa Kiwahabi na ugaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 26, 2016 03:11 UTC
  • Saleh: Hujuma dhidi ya Yemen ni uchokozi wa Mawahabi, magaidi

Ali Abdullah Saleh, mkuu wa chama cha Kongresi ya Kitaifa nchini Yemen ambaye pia ni rais wa zamani wa nchi hiyo, amesema kuwa, hujuma za Saudia dhidi ya nchi hiyo ni uchokozi wa Kiwahabi na ugaidi.

Ali Abdullah Saleh amewataka wavamizi wa Saudia kuondoka mara moja nchini humo kwa amani. Amesema, katika hali ya kushangaza ujumbe wa Riyadh haukufika katika mazungumzo ya Kuwait na badala yake umekuwa ukiahirisha mwenendo wa mazungumzo hayo. Amesema chama chake kinafanya juhudi kubwa kwa ajili ya kufikiwa maridhiano ya kitaifa nchini Yemen, huku akiwataja wavamizi hao wa Saudia kuwa watekelezaji wa siasa za kigaidi na za Kiwahabi katika mauaji yao nchini humo. Hii ni katika hali ambayo katika safari yake ya kiduru katika eneo la Mashariki ya Kati na katika fremu ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Yemen, Ban Ki-moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amefanya safari nchini Kuwait. Katika safari hiyo, Ban Ki-moon anatazamiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Ismail Ould Cheikh Ahmed, mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen. Mazungumzo ya Yemen nchini Kuwait yanawajumuisha wawakilishi wa Harakati ya Kiislamu ya Answarullah, chama cha Kongresi ya Kitaifa na ujumbe wa Abd Rabbuh Mansur Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyetangaza kujiuzulu na kukimbia nchi kuelekea Saudia.