-
Bin Salman ajibiwa: Kuvunjiwa heshima Haram Mbili Takatifu haliwi tena suala la ndani la Saudia
Nov 08, 2022 04:08Wanaharakati wa mitandao ya kijamii wamemjibu Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia aliyedai kwamba hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo kwa kumueleza kuwa kutusi na kuvunjia heshima nchi ambayo ndani yake kuna Haram mbili za Makka na Madina haliwi suala la ndani la Saudia.
-
Kiongozi wa HAMAS: Mazingira ya Ukingo wa Magharibi ni utangulizi wa kuutokomeza utawala wa Kizayuni
Nov 08, 2022 04:02Mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema mazingira ya hivi sasa katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni utangulizi wa kutokomezwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
-
Saudia yamhukumu kifo kijana kwa 'kosa' la kumuandalia futari mpinzani wa Ufalme
Nov 07, 2022 22:59Shirika moja la kimataifa la kutetea haki za binadamu limesema mahakama ya Saudia imetoa hukumu ya kifo kwa kijana mmoja kwa 'kosa' la kumuandalia futari mpinzani wa ufalme katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Kukaribia kumalizika muhula wa serikali ya muda ya Taliban nchini Afghanistan
Nov 07, 2022 22:57Msemaji wa serikali ya muda ya Taliban nchini Afghanistan amesema kipindi cha uongozi wa serikali hiyo kitamalizika baada ya muda si mrefu ujao.
-
Imran Khan: Maandamano ya kupinga serikali kuendelea tena kesho
Nov 07, 2022 09:13Imran Khan Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan amesema kuwa, maandamano ya kuipinga serikali kuelekea mji mkuu Islamabad yataendelea tena kesho Jumanne.
-
Msururu wa hukumu za vifo na kunyonga watu kwa halaiki; rekodi ya jinai aliyojiwekea Bin Salman
Nov 07, 2022 05:40Shirika la Haki za Kibinadamu la Saudi Arabia lenye makao yake Ulaya limefichua kuwa viongozi wa utawala wa Riyadh wametoa hukumu ya kifo kwa wafungwa 15 walioshtakiwa kwa masuala ya kiitikadi, na kwamba kwa kutolewa hukumu hizo, idadi ya watu walio hatarini kunyongwa nchini humo imefika 53, wanane miongoni mwao wakiwa ni vijana chipukizi na watoto wadogo.
-
Utawala wa Saudia wapanga kuwaua vijana 8 kutokana na tuhuma za ugaidi za uwongo
Nov 06, 2022 23:14Wanaharakati wa haki za binadamu wameonya kwamba Ufalme wa Saudi Arabia unapanga kuwanyonga vijana wanane kutoka eneo la Qatif lenye Waislamu wengi wa madhehebu ya Shia katika Mkoa wa Mashariki, huku ufalme huo wa kikoo unaoongozwa na Mwanamfalme Mohammed bin Salman ukishadidisha ukandamizaji dhidi ya wapinzani wanaotetea haki za kisiasa na kidini.
-
Jordan yaonya kuhusu hatua za Israel za kuzusha mizozo Palestina
Nov 06, 2022 23:14Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jordan ameonya kuhusiana na hatua za utawala haramu za Israel za kuzusha mivutano na mifarakano dhidi ya Wapalestina.
-
Safari ya Papa na mchezo mpya wa Al Khalifa; Uvumilivu kwa wasio Waislamu na ukatili dhidi ya Waislamu wa Bahrain
Nov 06, 2022 22:45Safari ya Kiongozi wa Kanisa katoliki Duniani, Papa Francis, nchini Bahrain kwa ajili eti ya kushiriki katika mkutano wa "Amani na Kuishi Pamoja" imefanyika katika hali ambayo hakushuhudiwi amani wala kuishi pamoja kwa usalama nchini Bahrain.
-
HAMAS: Msikiti wa Aqsa uko chini ya dhulma kubwa ya Wazayuni
Nov 05, 2022 22:49Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema kuwa, Msikiti wa al Aqsa (ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu) ni miongoni mwa nembo kuu ya Uislamu na kwamba mji mtakatifu wa Quds uliko Msikiti huo mtakatifu, daima umekuwa ukilengwa na maadui Wazayuni.