-
Udharura wa kufanyika mazungumzo ya kitaifa nchini Iraq
Sep 05, 2022 21:43Mustafa al-Kadhimi, Waziri Mkuu wa Iraq kwa mara nyingine ametoa wito wa kufanyika mazungumzo ya kitaifa kwa ajili ya kutatua matatizo ya nchi hiyo.
-
Wanajeshi wa Israel wamuua kijana Mpalestina katika Ukingo wa Magharibi
Sep 05, 2022 06:18Vikosi vya kijeshi vya utawala ghasibu wa Israel vimempiga risasi na kumuua shahidi kijana mwingine wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo siku ya Jumatatu.
-
Kununuliwa ardhi kwa ajili ya Wazayuni; juhudi za kuyahudishwa Manama
Sep 05, 2022 01:10Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya al-Wifah nchini Bahrain amesema kuna mpango wa siri unaotekelezwa kwa lengo la kuanzisha mtaa wa Mayahudi katika sehemu kongwe ya Manama, mji mkuu wa Bahrain.
-
UNICEF: Asia Magharibi inakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, Yemen imeathiriwa zaidi
Sep 04, 2022 22:01Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetahadharisha kuwa migogoro inayoendelea na kuzorota kwa hali ya kibinadamu katika nchi kadhaa za Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) na Kaskazini mwa Afrika (MENA) hususan Yemen kumewaacha mamilioni ya watu wakiwemo watoto katika hatari ya njaa.
-
Mcheza karate wa Kuwait akataa kucheza na Muisraeli mjini Baku
Sep 04, 2022 22:01Mpiganaji wa karate wa Kuwait Mohammad al-Otaibi amejiondoa katika mashindano ya 2022 ya Ligi Kuu ya Karate 1 katika mji mkuu wa Jamhuri ya Azerbaijan, Baku, ili kuepuka kukabiliana na mwakilishi wa utawala haramu wa Israel.
-
Mkuu wa zamani wa jeshi la Kizayuni: Israel haiwezi kuishambulia kijeshi Iran
Sep 04, 2022 06:07Mkuu wa zamani wa majeshi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel Shaul Mofaz amesema, Wairani ni watu werevu sana na wanao uwezo wa kuhakikisha wanapata haki zao za kinyukilia; na akakiri kwa kusema, Tel Aviv haina uwezo wa kuchukua hatua ya kijeshi dhidi ya Tehran.
-
Msafara wa baharini wa Lebanon waelekea mpaka wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu kulinda maliasili zake
Sep 04, 2022 06:06Msafara wa majini wa Lebanon umeanza safari yake ya kuelekea mpaka wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) kwa lengo la kulinda utajiri wa nchi hiyo wa maliasili za mafuta na gesi dhidi ya uporaji wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Wazayuni wazidisha jinai, waua shahidi makumi ya Wapalestina katika mwezi mmoja
Sep 04, 2022 02:32Takwimu zilizotolewa na vyombo vya habari vya Palestina zinaonesha kuwa utawala wa Kizayuni umeshadidisha jinai zake dhidi ya wananchi wasio na hatia kiasi kwamba katika mwezi mmoja tu ulioisha wa Agosti, Israel imeua shahidi Wapalestina 59 katika Ukanda wa Ghaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
CNN: Saudia inaelekea kuwa kitovu cha matumizi ya madawa ya kulevya Mashariki ya Kati
Sep 04, 2022 02:31Televisheni ya CNN ya Marekani imetangaza habari ya kukamatwa kete karibu milioni 47 za madawa ya kulevya nchini Saudi Arabia na kuongeza kuwa, nchi hiyo ya kifalme hivi sasa inaelekea kuwa kitovu cha matumizi ya mihadarati katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Manowari ya Uturuki yatia nanga katika bandari ya Haifa Palestina inayokaliwa kwa mabavu
Sep 03, 2022 21:54Vyombo vya habari vya Kiebrania vimeripoti kuwa manowari ya Uturuki pamoja na meli ya kivita ya kombora ya Marekani zimetia nanga katika bandari ya Haifa kaskazini-magharibi ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.