-
Kuwait: Tutaendelea kuisusia Israeli na makampuni yanayoshirikiana nayo
Aug 01, 2022 20:41Kuwait imetangaza kuwa itaendelea kuisusia Israel, bidhaa zake na makampuni yanayoshirikiana nayo. Hayo yametangazwa katika Mkutano wa Maafisa wa Ofisi za Kikanda za Kuisusia Israel.
-
Kuanza tena wimbi la kamatakamata huko Saudia baada ya safari ya kwanza ya Ulaya ya Muhammed bin Salman tangu mauaji ya Khashoggi
Aug 01, 2022 20:40Kufuatia ziara ya kwanza ya Ulaya ya mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman nchini Ugiriki na Ufaransa baada ya mauaji ya Jamal Khashoggi, ambayo imefanyika wiki mbili baada ya ziara ya Rais wa Marekani Joe Biden nchini Saudi Arabia, Shirika la Kudhibiti na Kupambana na Ufisadi la Saudi limetangaza habari ya kutiwa mbaroni maafisa 78 wa serikali kwa tuhuma za ufisadi, kula rushwa, utapeli, kutakatisha fedha na kutumia vibaya madaraka yao.
-
Uturuki kushirikiana na Syria dhidi ya wanamgambo wanaoungwa mkono na Marekani
Aug 01, 2022 00:00Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema kuwa nchi yake iko tayari kusaidia serikali ya Syria katika juhudi zake za kuwafurusha wanachama wa kundi la wanamgambo wa Kikurdi (YPG) wanaoungwa mkono na Marekani kutoka maeneo yenye utajiri wa nishati kaskazini mashariki mwa Syria.
-
Tawi la kijeshi la HAMAS lawaonyesha askari wawili wa Israel linaowashikilia mateka
Jul 31, 2022 07:10Brigedi za Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina, HAMAS zimetoa taswira, sambamba na kuwahutubu Wazayuni kwamba: viongozi wa utawala wa Kizayuni wanakuambieni uongo kuhusu mateka.
-
Sheikh Naim Qassem: Israel haina budi kutambua rasmi haki za maliasili za Lebanon
Jul 31, 2022 07:04Naibu Katibu MKuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel hauna budi kuzitambua rasmi haki za Lebanon zinazohusiana na utajiri wa maliasili za baharini.
-
Makumi ya viongozi wa serikali ya Saudia watiwa mbaroni kwa kula rushwa
Jul 31, 2022 02:55Serikali ya Saudi Arabia imewatia mbaroni maafisa 78 wa serikali kwa tuhuma za ufisadi, kula rushwa, utapeli, kutakatisha fedha na kutumia vibaya madaraka yao.
-
UN: Jela za siri za Imarati nchini Yemen zinatumiwa kutesa mahabusu
Jul 30, 2022 23:06Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi wake kuhusu ongezeko la ghasia na mateso katika jela za siri za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) huko Yemen.
-
Wafuasi wa mrengo wa Sadr wavamia tena jengo la Bunge la Iraq
Jul 30, 2022 23:01Wafuasi wa mrengo wa Sadr wamevamia tena kwa mara ya pili jengo la bunge la Iraq zikiwa zimepita chini ya siku tatu tangu walipovamia jengo hilo lililoko kwenye eneo lenye ulinzi mkali katikati ya mji mkuu wa nchi hiyo Baghdad.
-
Mgogoro Iraq; Bunge lavamiwa huku nara zikipigwa dhidi ya Waziri Mkuu aliyependekezwa
Jul 30, 2022 23:01Mamia ya wananchi wa Iraq tarehe 27 mwezi huu wa Julai waliandamana katika Eneo la Kijani katika mji mkuu Baghdad na kisha wakavamia Bunge na kupiga nara na shaari dhidi ya mwanasiasa aliyependekezwa kwa ajili ya nafasi ya Waziri Mkuu.
-
Macron akosolewa kwa 'kumtandikia zulia jekundu muuaji wa Khashoggi'
Jul 29, 2022 23:16Wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu wamemkosoa vikali Rais Emmanuel Macron wa Ufarasa kwa kumpokea Mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, ambaye anatuhumiwa kutoa amri ya kuuawa mwanahabari Jamal Khashoggi, huko nchini Uturuki miaka 4 iliyopita.