Moscow: Marekani inawafanya Waafrika kuwa 'panya wa maabara'
Mkuu wa Kikosi cha Ulinzi wa Kibaolojia cha Russia amefichua kuwa Marekani inawafanya Waafrika kuwa panya wa maabara na kwamba inawatumia watu wa bara hilo kufanyia majaribio dawa za kemikali.
Igor Krylov amesema, nyaraka zilizogunduliwa nchini Ukraine zinaonyesha kuwa Pentagon inapanga kutumia maabara zake za siri barani Afrika kufanyia majaribio dawa ambazo hazijasajiliwa kwa kutumia wakazi wa bara hilo.
Krylov ameendelea kusema kuwa, nyaraka zilizopatikana huko Ukraine zinaonyesha kuwa Shirika la Kupunguza Vitisho vya Ulinzi la Marekani (DTRA), Wizara ya Usalama wa Taifa, pamoja na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani na taasisi kadhaa za Umoja wa Ulaya zinahusika katika utafiti wa vimelea vya maradhi katika nchi za Afrika.
Krylov amesema: "Tumesema mara kwa mara kwamba kuna mahusiano baina ya kampuni hii, Hunter Biden, mtoto wa rais wa sasa wa Marekani, na mashirika ya serikali."
Ameongeza kuwa, Kituo cha Sayansi na Teknolojia cha Ukraine na wakandarasi wengine wa Pentagon wanahusika kikamilifu katika shughuli hizi.
Tangu 1942, Marekani ilianza mpango wa utengenezaji wa silaha za kibaolojia, na ndio nchi pekee iliyowahi kutumia silaha za atomiki kuangamiza wanaadamu dunia.
Mapema mwezi Aprili mwaka huu Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lilitangaza kuwa linachunguza uwezekano wa kuwepo kwenye soko poda za watoto zinazotengenezwa na kampuni kubwa ya dawa ya Marekani, Johnson & Johnson (J&J), ambazo imebainika kuwa zinasababisha saratani.

Makampuni ya Marekani yana historia mbaya ya kujaribu au kuuza dawa na bidhaa zenye madhara kwa binadamu hususan katika nchi zinazoendelea. Kwa mfano kampuni ya Kimarekani ya Pfizer ilifanya majaribio ya dawa mpya ya antibiotiki, Trovan, katika jimbo la Kano kaskazini mwa Nigeria mwaka 1996.
Mgogoro wa kisheria wa muda mrefu uliibuka na hatimaye kampuni hiyo kubwa ya kutengeneza dawa ikalazimika kuwalipa fidia wazazi ambao watoto wao walishirikishwa katika majaribio ya dawa hiyo wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa utindio wa ubongo. Watoto 11 walifariki dunia na makumi ya wangine kupooza baada ya kupewa dawa ya kuzuia maumivu iliyokuwa ikifanyiwa majaribio na shirika hilo la Kimarekani.