Sep 20, 2023 07:44 UTC
  • Kuendelea  vita vya maneno vya Trump dhidi ya Rais wa Marekani

Rais wa zamani wa Marekani, amekejeli hotuba ya jana ya Rais Joe Biden wa nchi hiyo katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ikiwa ni katika kuendelea na mashambulizi yake ya maneno na ukosoaji dhidi ya kiongozi huyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Donald Trump rais wa zamani wa Marekani, siku ya Jumanne alikosoa jinsi Joe Biden alivyozungumza kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kusema nchi hiyo imepoteza heshima yake duniani.

Trump ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa "Truth Social" kuwa Biden hivi punde amemaliza  hotuba yake ya kusalimu amri katika Umoja wa Mataifa na hakuna aliyehudhuria kikao hicho licha ya Marekani kutoa kila kitu kwao. Akirejelea ukweli kwamba idadi kubwa ya viti vya viongozi wa nchi tofauti vilikuwa tupu wakati wa hotuba ya Biden, Trump amekiri kuwa Marekani haiheshimiwi tena ulimwenguni. 

Hivi karibuni, Rais huyo wa zamani wa Marekani alikiri kwamba Marekani ilikuwa imepoteza heshima yake duniani.

Trump pia amekariri madai yake kuhusu udanganyifu uliofanyika katika uchaguzi wa rais wa 2020 wa Marekani, ambao Biden alitangzwa kuwa mshindi.

Akiashiria majanga kama vile mfumuko wa bei ya vyakula na kuyumba uchumi wa Marekani kutokana na uungaji mkono wake kwa vita vya Ukraine, Trump amesema: Marekani halisi ni ile iliyokuwepo zamani.

Awali, rais huyo wa zamani wa Marekani alifichua katika mahojiano yenye utata kwamba Marekani si tu kuwa si nchi yenye nguvu kubwa tena, bali inaelekea kuzimu. Alisema kupungua kwa ushawishi wa sarafu ya dola duniani ni "tukio kubwa kuliko kushindwa kwa vita vyovyote vile".

Tags