Dec 23, 2023 07:54 UTC
  • City yatwaa ubingwa Kombe la Dunia kwa Klabu+VIDEO

Manchester City ya Uingereza imeibuka kidedea na kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia kwa Klabu kwa mara ya kwanza, na hivyo kuidhihirishia dunia kwa mara nyingine tena kuwa ndiyo klabu bora zaidi duniani.

Man City imeifunga klabu ya Fluminense (Flu) ya Brazil mabao 4-0 katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo ambayo kila bara linawakilishwa na timu moja iliyotwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa kwa bara husika.

Katika mchezo huo wa Ijumaa uliopigwa katika Uwanja wa Mwanamfalme Abdullah Al-Faisal uliopo mjini Jeddah nchini Saudi Arabia, mabao ya City yalifungwa na Phil Foden, Julian Alvarez mawili na moja lakujifunga.

Msimu uliopita City ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka ya Uingereza EPL, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la FA, UEFA Super Cup, na FIFA CLUB World Cup.

Al Ahly walioshinda Klabu Bingwa Afrika miezi 6 iliyopita, wamembulia nafasi ya 3 Kombe la Dunia

Wakati huohuo, klabu ya Al Ahly ya Misri imemaliza nafasi ya tatu kwenye mashindano hayo ya Kombe la Dunia kwa klabu baada ya kuifunga Urawa Red Diamonds kwa mabao 4-2.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Mwanamfalme Abdullah Al-Faisal uliopo mjini Jeddah nchini Saudi Arabia, mabao ya Al Ahly yalifungwa na Yasser Ibrahim 19', Perce Tau 25', Yasser Ibrahim akijifunga katika dakika ya 60, na Ali Maaloul akifunga akaunti ya mabao dakika ya 90+.

Mabao mawili ya kufutia machozi ya Urawa Red Diamonds yalifungwa na wachezaji José Kante dakika ya 43 na Alexander Scholz akifunga dakika ya 54.

 

Tags