NATO yaanza mazoezi ya kijeshi baharini karibu na Russia
Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) umeanza mazoezi ya kijeshi karibu kabisa na Russia.
Mazoezi hayo ya NATO yanaenda sambamba na kuanza kwa mazoezi mengine ya majaribio ya makombora ya Russia maarufu kwa jina la 'Intercontinental' yanahudhuriwa na askari wa nchi kadhaa za Bahari Nyeusi ikiwemo Russia.
Mazoezi hayo ya NATO ambayo yamepewa jina la 'SEA BREEZE 2016' yanazijumuisha meli 25 za kivita, meli za misaada ya kivita na vikosi vya baharini vya NATO. Mazoezi hayo ya kijeshi ya wiki moja yanawajumuisha askari wa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) kutoka nchi wanachama zikiwemo, Romania, Bulgaria, Uturuki na Uhispania. Baada ya NATO kutangaza uamuzi wake wa kutuma askari karibu na mipaka ya Russia, serikali ya Moscow nayo kwa upande wake imetangaza kuanza mazoezi makubwa zaidi ya makombora yake yanayovuka mabara na kulenga shabaha umbali wa kilomita elfu 8.
Katika mazoezi hayo ya makombora, Russia imeweka tayari silaha zake nzito yakiwemo makombora ya Topol, Topol-M 1 na Yars wenye uwezo wa kupiga umbali wa kilometa 8000.