Mbunge wa Marekani: Biden ni punguani, hana akili timamu
Wawakilishi wawili wa Marekani wamekosoa vikali uamuzi wa Joe Biden wa kuondoa vikwazo kwa Kiev vya kutumia silaha za Marekani kushambulia ardhi ya Russia.
Tovuti ya habari ya Politico imeripoti habari hiyo kwa kuwanukuu wabunge maafisa wawili wa utawala wa Joe Biden wakisema kwamba serikali ya Marekani iliidhinisha kwa siri jeshi la Ukraine kutumia silaha za Marekani kushambulia ardhi ya Russia.
Kwa upande wake, shirika wa habari la IRNA limeripoti kuwa, Mbunge wa Marekani Marjorie Taylor Green amesema kuwa, Joe Biden ni kichaa kwa uamuzi wake wa kuondoa vikwazo vya Kiev kutumia silaha za Marekani kushambulia ardhi ya Russia.
Taylor Greene ameongeza kwamba Joe Biden ameidhinisha kwa siri Ukraine kuivamia ardhi ya Russia kwa silaha za Marekani uamuzi ambao unazidisha mvutano ambao unaweza kutupelekea kuingia moja kwa moja katika vita na Russia.
Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Marekani aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba Joe Biden si tu ni mwenye akili dhaifu, lakini pia ni mwendawazimu. Marekani inapaswa kujitahidi kuleta amani si vita vya dunia.
Mbunge mwingine wa Marekani Matt Gates naye amesema kuwa uamuzi wa Joe Biden wa kuiondolea Kiev marufuku ya matumizi ya silaha za Marekani kushambulia ardhi ya Russia unaweza kusababisha Vita vya Tatu vya Dunia.
Matt Gates aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba matumizi ya Kiev ya silaha za Marekani yanauweka ulimwengu katika hatari ya Vita vya Tatu vya Dunia.
Kutoheshimu utawala wa Joe Biden Rais wa Marekani kwenye suala hili ni jambo la kutisha na Sera za Marekani zimekuwa kwamba Ukraine haiwezi kutumia silaha za Marekani kushambulia ardhi ya Russia.
Katika wiki za hivi karibuni Marekani ilituma kwa siri makombora ya masafa marefu ya (ATACMS) kwa Ukraine kwa matumizi katika vita na Russia na Ukraine iliyatumia kwa mara ya kwanza wiki iliyopita.