Jun 14, 2024 07:32 UTC
  • Waziri Mkuu wa Uhispania ayataka mataifa ya Ulaya kuitambua rasmi Palestina

Pedro Sanchez, Waziri Mkuu wa Uhispania ameyataka mataifa ya Ulaya kuitambua rasmi Palestina kama nchi na dola huru.

Waziri Mkuu wa Uhispania ametoa wito huo katika mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa nchi hiyo Madrid akiwa pamoja na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na kusisitiza kuwa, anayatolea mwito mataifa yote ya Ulaya kulitambua rasmi taifa la Palestina.

Sanchez ameeleza kuwa, kutambuliwa taifa huru la Palestina ndio suluhisho pekee la kusimamisha jinai za utawala wa Kizayuni na akatangaza juhudi za Madrid za kusimamisha vita huko Gaza.

Kwa upande wake Rais Erdogan wa Uturuki sambamba na kusifu hatua ya Uhispania ya kutambua rasmi taiifa la Palestina amesema nchi yake iko tayari kushirikiana na taifa hilo kuipatia ufumbuzi kadhia ya Gaza.

Pedro Sanchez, Waziri Mkuu wa Uhispania 

 

Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez amewahi kuusiisitiza mara kadhaa kwamba, kutambuliwa rasmi taifa la Palestina ni muhimu kwa amani, akisisitiza kwamba hatua hiyo haijachukuliwa dhidi ya Israel na kwamba ndiyo njia pekee ya kuhakikisha mustakabali wa mataifa mawili yanayoishi bega kwa bega kwa amani na usalama.

Mwishoni mwa mwezi uliopita wa Mei Uhispania, Ireland na Norway zilipasisha rasmi mpango wa kutambua rasmi Palestina, katika uamuzi ulioratibiwa hatua ambayo imeongeza himaya na uungaji mkono kwa Palestina barani Ulaya.

Tags