Jun 17, 2024 02:58 UTC
  • Russia yatungua makumi ya droni, maroketi ya Ukraine

Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa imetungua maroketi na ndege kadhaa zisizo na rubani za Ukraine (droni) ndani ya saa 24.

Shirika la habari la Press TV limetangaza kuwa, Wizara ya Ulinzi ya Russia imetoa taarifa na kutangaza kuwa kikosi cha ulinzi wa anga cha jeshi la nchi hiyo kimenasa na kuziharibu ndege zisizo na rubani 54 za jeshi la Ukraine.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, idadi kadhaa ya maroketi ya HIMARS ya jeshi la Ukraine yamedhibitiwa na kutwaliwa na jeshi la Russia katika operesheni hiyo. Kadhalika kikosi cha ulinzi wa anga cha jeshi la kimefanikiwa kuharibu mabomu kadhaa ya kuelekezwa ya jeshi la Ukraine.

Mkuu wa Majeshi ya Ukraine ametangaza kuwa, vikosi vya nchi hiyo vimepigana vita 74 na Russia katika maeneo tofauti katika muda wa saa 24.

Amesema vikosi vya Russia vimeendelea kufanya hujuma za anga dhidi ya maeneo mbali mbali ya Ukarine hasa katika eneo la Pokrovsk. Amedai kuwa wanajeshi wa Ukraine wamefanikiwa kuzima aghalabu ya mashambulio ya Russia.

Hii ni katika hali ambayo, Rais Vladimir Putin wa Russia anasisitiza kuwa, mzozo wa Ukraine utamalizika kwa kukubaliwa matakwa na masharti ya nchi yake.

 

 

 

Tags