IOM yakosoa matamshi ya Trump dhidi ya wageni
https://parstoday.ir/sw/news/world-i11845-iom_yakosoa_matamshi_ya_trump_dhidi_ya_wageni
Shirika la Kimataifa la Wahajiri (IOM) limeeleza wasiwasi wake kuhusu matamshi yaliyotolewa na mgombea kiti cha rais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Ttrump kuhusu raia wa kigeni na kusema matamshi hayo yanachochea chuki dhidi ya wageni.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 24, 2016 02:52 UTC
  • IOM yakosoa matamshi ya Trump dhidi ya wageni

Shirika la Kimataifa la Wahajiri (IOM) limeeleza wasiwasi wake kuhusu matamshi yaliyotolewa na mgombea kiti cha rais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Ttrump kuhusu raia wa kigeni na kusema matamshi hayo yanachochea chuki dhidi ya wageni.

Joel Millman amesema kuwa, misimami ya Trump inazidisha chuki na hisi za kuwapiga vita raia wa kigeni na kwamba kuwadhihirisha wahajiri halali na haramu kuwa ni mashetani na watu waovu kutazidisha matatizo ya wahajiri hao. 

Vilevile amekosoa fikra iliyotolewa na mgombe huyo wa kiti cha rais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican aliyetoa pendekezo la kujengwa ukuta wa kuzuia wahamiaji kuingia Marekani katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico. 

Katika hotuba yake ya Ijumaa iliyopita Donald Trump alisisitiza tena msimamo wake wa kuzuia wahajiri kuingia Marekani na kutoa tena pendekezo la kujengwa ukuta katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico. 

Vilevile Trump amekuwa akitoa matamshi ya kibaguzi dhidi ya Waislamu na ametoa pendekezo la kutumiwa mbinu za kikatili za kipindi cha utawala wa dikteta wa zamani wa Ujerumani, Adolph Hitler dhidi ya Waislamu nchini Marekani.