Katibu Mkuu UN: Natiwa wasiwasi na kushtadi mivutano huko Syria
-
Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi wake juu ya kuongezeka hali ya mvutano kati ya makundi yenye silaha nchini Syria na wapiganaji wa Kikurdi.
Katika mazungumzo ya simu na Fuad Hussein, Waziri wa Mashauri ya Kigeni na Naibu Waziri Mkuu wa Iraq, Antonio Guterres amesisitiza kuwa umoja huo utaendelea kuwasiliana na Uturuki na Qatar ili kutuliza hali ya mambo huko Syria.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iraq pia ameeleza kuwa, hali ya sasa ya Syria ni tete baada ya makundi mbalimbali yenye silaha kudhibiti maeneo mengi ya nchi hiyo, na kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) kuanza tena kuwakusanya wapiganaji wake kwa kutumia vibaya hali ya mchafukoge kufuatia kusambaratika jeshi la Syria na kurudi nyuma wapiganaji wa Kikurdi kuelekea mashariki mwa mto Furat.
Fuad Hussein amesisitiza udharura wa kudhaminiwa usalama jamii ya raia waliowachache wa Syria na kuhakikisha kuwa jamii hiyo inashirikishwa katika mchakato wa kisiasa na hawahamishwi kwa nguvu, na haki zao zinalindwa katika fremu ya serikali jumuishi ya makundi yote.
Kwa sasa, Syria haina serikali umoja na sehemu nyingi za nchi hiyo zimekaliwa kwa mabavu na wanajeshi wa Israel, Marekani na Uturuki.