CNN: Dalili za kuporomoka uchumi wa Marekani ziko wazi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i123768-cnn_dalili_za_kuporomoka_uchumi_wa_marekani_ziko_wazi
Tovuti ya CNN imeashiria katika makala yake kuhusu kuongezeka idadi ya watu walioachishwa kazi, kupungua mchakato wa kuajiri watu, mfumuko wa bei n.k nchini Marekani na kusisitiza kuwa sera za ushuru za Rais Donald Trump wa nchi hiyo zimezidisha matatizo ya kiuchumi nchini humo.
(last modified 2025-03-11T03:39:35+00:00 )
Mar 11, 2025 03:39 UTC
  • CNN: Dalili za kuporomoka uchumi wa Marekani ziko wazi

Tovuti ya CNN imeashiria katika makala yake kuhusu kuongezeka idadi ya watu walioachishwa kazi, kupungua mchakato wa kuajiri watu, mfumuko wa bei n.k nchini Marekani na kusisitiza kuwa sera za ushuru za Rais Donald Trump wa nchi hiyo zimezidisha matatizo ya kiuchumi nchini humo.

Mchezo wa kuongezeka ushuru wa Rais Donald Trump na hasa kutoaminika hatua anazochukua kuhusu suala hilo vimesababisha mkanganyiko kwa wafanyabiashara wa Marekani, watumiaji na wawekezaji; jambo ambalo limezua wasiwasi kuhusu mfumuko wa bei wa bidhaa mbalimbali za matumizi. 

Televisheni ya CNN imeongeza kuwa: Hatua ya Trump ya kuwakandamiza wahajiri inatishia viwanda muhimu vikiwemo vya kilimo, ujenzi na huduma za afya. Katika upande mwingine, kupungua pakubwa idadi ya wafanyakazi wa shirikisho na misaada ya serikali kunaweza kuwaathiri na kuwaumiza Wamarekani walio hatarini zaidi ambao hawana hata kinga ndogo mkabala wa mfumuko wa bei unaoisibu nchi hiyo. 

Kwa mujibu wa uchambuzi huu, sera za Trump zinahatarisha sana uchumi ambao umetajwa kuwa chanya kwa kiwango fulani lakini uliolegalega aliorithi. Kitengo cha Biashara cha Marekani kimeeleza kuwa, matumizi ya watumiaji yalipungua bila kutarajiwa Januari mwaka huu, huku wananchi wakipunguza manunuzi yao kinyume na ilivotarajiwa na wachumi.