Vita vya Iran na Israel vyasambaa hadi katika ligi ya soka ya Argentina
(last modified Tue, 01 Jul 2025 02:32:59 GMT )
Jul 01, 2025 02:32 UTC

Mashabiki wa timu ya soka katika Ligi ya Argentina, katika mkesha wa mechi dhidi ya timu nyingine inayowakilisha Wayahudi wa nchi hiyo, wamekaribisha mechi hiyo kkwa kupeperusha bendera za Iran na Palestina.

Kabla ya mechi kati ya timu za daraja la pili, Club Atlético All Boys na Atlanta, ambayo inawakilisha jamii ya Wayahudi nchini Argentina, mashabiki wa All Boys waliandamana kwa kupeperusha bendera za Iran na Palestina na kuchoma moto jeneza lenye bendera ya Israel.

Katika mkutano huo, mashaka kadhaa, waliovalia mavazi ya usalama yaliyoundwa kustahimili vitisho vya hujuma za silaha za vijidudu na kemikali, walibeba jeneza lenye bendera ya Israeli huku moshi mweusi ukitoka kwenye jeneza hilo.

Mashabiki wengine waliovalia mavazi kama hayo, pia walipeperusha bendera za Irani na Palestina. Hatua hii ya kiishara imekuja kufuatia vita vya siku 12 vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani dhidi ya Iran.

Baadhi ya mashabiki wa Club Atlético All Boys waliimba na kutoa kauli mbiu kama vile "Free... Free Palestine."