Venezuela yalaani uamuzi wa utawala wa Kizayuni wa kuukalia kwa mabavu Ukanda wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/world-i129340
Serikali ya Venezuela imepinga vikali mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuukalia kwa mabavu Ukanda wa Gaza na kuitaja hatua hiyo kuwa ni kuzidisha mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina.
(last modified 2025-08-09T13:30:42+00:00 )
Aug 09, 2025 13:30 UTC
  • Yvan Eduardo Gil
    Yvan Eduardo Gil

Serikali ya Venezuela imepinga vikali mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuukalia kwa mabavu Ukanda wa Gaza na kuitaja hatua hiyo kuwa ni kuzidisha mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela, Yvan Eduardo Gil amesema kuwa, mpango huu wa kutaka kuikalia kwa mabavu Gaza unalenga kufuta uwepo wa watu wa Palestina na hauwezi kuvumiliwa na dhamiri ya ubinadamu.

Serikali ya Caracas imetaka kutiwa mbaroni mara moja viongozi husika wa Israel katika ngazi ya kisiasa, kiuchumi na  kidiplomasia na kuitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua kali na za haraka dhidi ya uamuzi wa Israel. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela amesisitiza kuwa, miaka miwili iliyopita, sera za kutenda jinai za Israel zimepelekea kuuliwa raia zaidi ya elfu 60, kubomolewa kikamilifu makazi ya watu, mamilioni ya watu kuwa wakimbizi, kuharibiwa miundombinu muhimu na kuwekwa mzingiro usio wa kibinadamu ambao lengo lake ni kuangamiza maisha ya watu huko Palestina. 

Wakati huo huo nchi mbalimbali zimeendelea kutoa radiamali  zikipinga mpango ulioidhinishwa na baraza la mawaziri la kisiasa na kiusalama la utawala haramu wa Israel  wa kulikalia kwa mabavu eneo lote la Ukanda wa Gaza. Serikali ya Chile pia imelaani vikali azimio la karibuni la baraza la mawaziri la usalama la Israel la kuikalia Gaza kwa mabavu, ikitaja hatua hiyo kuwa ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na tishio la kuzidisha mgogoro wa binadamu, kisiasa na kiusalama katika eneo hilo.