Russia yakosoa vitisho vya Marekani dhidi ya Iran yasema 'havikubaliki'
https://parstoday.ir/sw/news/world-i136212-russia_yakosoa_vitisho_vya_marekani_dhidi_ya_iran_yasema_'havikubaliki'
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ruussiia amesoa vitisho vya Marekani dhidi ya Iran akisema 'havikubaliki' huku Moscow ikitaka kupunguzwa mashinikizo ya Marekani dhiidi ya Iran.
(last modified 2026-02-03T09:29:02+00:00 )
Feb 03, 2026 09:29 UTC
  • Sergei Lavrov
    Sergei Lavrov

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ruussiia amesoa vitisho vya Marekani dhidi ya Iran akisema 'havikubaliki' huku Moscow ikitaka kupunguzwa mashinikizo ya Marekani dhiidi ya Iran.

Sergei Lavrov amelaani vitisho vipya vya Marekani vya kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran, akionya kwamba kitendo chochote kipya cha uchokozi kitakuwa na matokeo mabaya kikanda na kimataifa.

Katika majibu ya maandishi yaliyoandaliwa kwa ajili ya mkutano na waandishi wa habari, Lavrov pia ametilia mkazo juhudi za Moscow za kupunguza mvutano na kuondoa mashinikizo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

"Vitisho vya mashambulizi mapya ya kijeshi dhidi ya ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu havikubaliki kabisa," amesisitiza Sergei Lavrov, akionya kwamba kurudia uchokozi wowote wa kijeshi kutakuwa na "matokeo mabaya" kwa eneo la Asia Magharibi na usalama wa kimataifa.

Lavrov pia ameonya dhidi ya kutumia "machafuko yanayochochewa na wageni" kama kisingizio cha kukariri "uchokozi dhidi ya Iran kama ule uliofanywa Juni 2025," akisisitiza kwamba vitendo kama hivyo vitadhoofisha sana usalama wa kimataifa.

Makundii ya watu waliokuwa na silaha na magaidi wanaoungwa mkono na nchi za kigeni waliteka nyara maandamano ya amani kuhusu malalamiko ya kiuchumi mnamo Januari 8 na 9 na kusababisha ghasia na mauaji ya raia wasio na hatia.

Wakati huo Rais wa Marekani Donald Trump alihimiza vurugu hizo hadharani na waziwazi kwa kuwataka mamluki waliokuwa na silaha kutwaa taasisi za serikali na kutishia kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran kama itakabiliana na ghasia hizo.