Utafiti wa Fox News: Trump hana afya ya akili
https://parstoday.ir/sw/news/world-i137948-utafiti_wa_fox_news_trump_hana_afya_ya_akili
Asilimia 60 ya washiriki katika utafiti wa Fox News, kituo kinachomuunga mkono rais wa Marekani, wamesema kuwa Donald Trump hana tabia na afya ya akili inayofaa.
(last modified 2026-04-25T11:07:19+00:00 )
Apr 25, 2026 11:04 UTC
  • Donald Trump
    Donald Trump

Asilimia 60 ya washiriki katika utafiti wa Fox News, kituo kinachomuunga mkono rais wa Marekani, wamesema kuwa Donald Trump hana tabia na afya ya akili inayofaa.

Fox News imeashiria utafiti uliofanywa wiki iliyopita na kuripoti kuwa asilimia 56 ya wananchi wa Marekani wana shaka juu ya uwezo wa Trump kuongoza serikali.

Pia, asilimia 60 ya washiriki katika utafiti huo wamesema kuwa Trump hana tabia na afya ya akili inayofaa kwa nafasi yake, kiwango ambacho kimeongezeka takriban kwa asilimia 10 ikilinganishwa na kabla ya kipindi chake cha sasa cha urais. 

Utafiti huo pia umeonyesha kushuka imani ya Wamarekani kwa utendaji wa baraza la mawaziri la Donald Trump, ambapo JD Vance, makamu wa rais, Mark Rubio, waziri wa mambo ya nje, na Pete Hegseth, waziri wa vita wa Marekani, wamepata ongezeko la alama hasi kati ya asilimia 11 hadi 17.

Sera za nje, vita dhidi ya Iran, uchumi, matumizi ya serikali, na jinsi serikali inavyowatendea wahamiaji zimeelezwa kuwa sababu kuu za kuongezeka mitazamo hasi ya Wamarekani kuhusu serikali yao.