Rais wa Venezuela aliyetekwa akanusha mashtaka yanayomkabili Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i142226-rais_wa_venezuela_aliyetekwa_akanusha_mashtaka_yanayomkabili_marekani
Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, amekanusha mashtaka mapya ya utesaji yaliyotolewa dhidi yake na Marekani katika mahakama ya New York.
(last modified 2026-10-16T09:13:07+00:00 )
Oct 16, 2026 09:10 UTC
  • Rais wa Venezuela aliyetekwa akanusha mashtaka yanayomkabili Marekani

Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, amekanusha mashtaka mapya ya utesaji yaliyotolewa dhidi yake na Marekani katika mahakama ya New York.

“Hizi ni tuhuma za uongo dhidi yangu,” Maduro alimwambia jaji kupitia mkalimani wa Kihispania Alhamisi.

Maduro, ambaye amekuwa rais wa Venezuela aliyechaguliwa kidemokrasia tangu mwaka 2013 hadi kutekwa kwake na vikosi vya kijeshi vya Marekani katika uvamizi wa usiku mwezi Januari 2026, kwa sasa anazuiwa katika gereza la kuogofya la New York.

Anakabiliwa na hati ya mashtaka iliyofanywa upya inayopanua mashtaka ya awali ya usafirishaji wa madawa ya kulevya ili kujumuisha mashtaka ya utesaji, yaliyowasilishwa na utawala dhalimu wa Marekani.

Maduro, pamoja na mke wake, Mwanasheria Mkuu wa awali, Cilia Flores , ambao wote wawili walifikishwa mahakamani wakiwa wamefungwa pingu vifungoni , hivi karibuni walishtakiwa kwa kuongoza kampeni ya kiserikali ya ukandamizaji na kuwatesha watu kadhaa, ikiwa ni pamoja na Wamarekani watatu.

Rais huyo wa Venezuela alimwambia Jaji wa Manhattan, Alvin K. Hellerstein, kwamba shutuma hizo ni “tuhuma za uongo na ushuhuda wa uongo.”

Jaji Hellerstein alikerwa sana na kauli ya Maduro na akaamua kuchukua hatua mwenyewe, akijitokeza na kusema kwamba “kauli ya kuwa au kutokuwa na hatia itaamuliwa kwa niaba ya Maduro.”

Mke wa Maduro,Flores hakusema mengi, akimwambia jaji kupitia mkalimani: “Sina hatia kabisa. Sina hatia.”

Maduro amekanusha vikali mashtaka dhidi yake na kusisitiza kuwa utekwaji wake ni tokeo la moja kwa moja la hamu ya kibabe ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kutaka kuidhibiti akiba kubwa ya mafuta na gesi asilia ya nchi hiyo ya Amerika ya Kusini.

Mawakili wao wanasistiza kwamba kesi zinazowakabili Maduro na Flores lazima zifutwe kwa sababu za kinga ya diplomasia, kwani ni rais na mke wa rais (first lady) wa taifa huru la kigeni.

Licha ya hoja za upande wa utetezi, jaji aliidhinisha ratiba inayoweka kuanza kwa kesi hiyo tarehe 14 Juni 2027.