Maelfu waandamana Brazil kumuunga mkono Rais Rousseff aliyeuzuliwa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i14653-maelfu_waandamana_brazil_kumuunga_mkono_rais_rousseff_aliyeuzuliwa
Maelfu ya watu wameandamana nchini Brazil kumuunga mkono rais aliyeuzuliwa Bi. Dilma Rousseff huku wakibainisha upinzani wao kwa serikali mpya inayoongozwa na Michel Temer.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Sep 05, 2016 07:24 UTC
  • Maelfu waandamana Brazil kumuunga mkono Rais Rousseff aliyeuzuliwa

Maelfu ya watu wameandamana nchini Brazil kumuunga mkono rais aliyeuzuliwa Bi. Dilma Rousseff huku wakibainisha upinzani wao kwa serikali mpya inayoongozwa na Michel Temer.

Wafuasi wa Rousseff wametaja hatua ya Temer kuchukua madaraka kuwa ni mapinduzi  na wametaka uchaguzi mpya uitishwa ncini humo.

Waandamanaji zaidi ya laki moja walimiinika katika mji wa Sao Paulo huki wakimtaka Temer aondoke madarakani.

Jumatano iliyopita, Bunge la Senate nchini Brazil lilimpata Rousseff na hatia ya ubadhirifu wa fedha za umma na hivyo kumuondoa madarakani na nafasi yake imechukuliwa na hasimu wake wa kisiasa, Temer ambaye aliwahi kuwa makamu wa rais.

Dilma Rousseff (kushoto) na Michel Temer

Viongozi wa mrengo wa kushoto nchini Brazil wanasema kiini cha migogoro ya eneo hilo kinatokana na uingiliaji wa kigeni. Kwa mujibu wa viongozi hao, matukio yote yanasababishwa na siasa chafu za Marekani katika eneo la Amerika ya Latini.

Kwa mujibu wa viongozi hao wa mrengo wa kushoto nchini Brazil, uchochezi wa Marekani katika kuuzuliwa Rais Dilma Rousseff, si jambo jingine ila ni kukabiliana na matakwa ya wananchi wanaotaka uhuru na kujitegemea.