Miili kumi ya wahajiri yapatikana kwenye boti katika maji ya Libya
https://parstoday.ir/sw/news/world-i18910-miili_kumi_ya_wahajiri_yapatikana_kwenye_boti_katika_maji_ya_libya
Kikosi cha ulinzi katika pwani ya Italia kimeripoti kuwa kimepata miili ya wahajiri kumi walioaga dunia ikiwa ndani ya boti katika maji ya Libya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 06, 2016 04:32 UTC
  • Miili kumi ya wahajiri yapatikana kwenye boti katika maji ya Libya

Kikosi cha ulinzi katika pwani ya Italia kimeripoti kuwa kimepata miili ya wahajiri kumi walioaga dunia ikiwa ndani ya boti katika maji ya Libya.

Kikosi cha ulinzi katika pwani ya Italia kimeeleza kuwa wahamiaji haramu zaidi ya 2100 wameopolewa majini kufuatia oparesheni kadhaa zilizofanywa jana katika maji ya Mediterania na kwamba miili ya wahajiri wengine kumi walioaga dunia pia imepatikana kwenye oparesheni hiyo. Kikosi hicho kimeongeza kuwa, oparesheni 8 za uokoaji zilifanywa juzi katika maji ya Mediterania ambapo wahajiri 1200 waliokolewa.

Wafanyakazi wa uokoaji wa Italia wakiwa katika oparesheni za kuwaokoa wahajiri wa Kiafrika

Katika miaka ya hivi karibuni Libya imegeuka na kuwa sehemu ya kupitishia wahajiri kuelekea katika nchi za Ulaya kutokana na nchi hiyo kuwa karibu na Italia. Wafanya biashara wa magendo ya binadamu pia wanatumia vibaya hali hiyo kwa kuwasafririsha wahajiri kupita kiasi katika boti zao na kusababisha maafa makubwa ya kibinadamu. Mwaka huu wa 2016 wahajiri 3740 wamepoteza maisha katika bahari ya Mediterania. Shirika la Amnesty International juzi liliituhumu polisi ya Italia kuwa inatumia mabavu kuamiliana na wahajiri wa Kiafrika wanaojaribu kuingia nchini humo.