Viongozi wa Waislamu Marekani wamwandikia barua ya wazi Trump
https://parstoday.ir/sw/news/world-i20884-viongozi_wa_waislamu_marekani_wamwandikia_barua_ya_wazi_trump
Shakhsia wapatao 300 wa Kiislamu nchini Marekani wamemwandikia barua ya wazi Rais mteule wa nchi hiyo Donald Trump likiwa ni jibu kwa matamshi ya chuki aliyotoa dhidi ya Uislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 06, 2016 12:13 UTC
  • Viongozi wa Waislamu Marekani wamwandikia barua ya wazi Trump

Shakhsia wapatao 300 wa Kiislamu nchini Marekani wamemwandikia barua ya wazi Rais mteule wa nchi hiyo Donald Trump likiwa ni jibu kwa matamshi ya chuki aliyotoa dhidi ya Uislamu.

Shakhsia 291 wakiwemo wajumbe wakuu wa Baraza la Mahusiano ya Marekani na Uislamu (CAIR), maimamu wa misikiti, wahadhiri wa vyuo vikuu, wanaharakati pamoja na wakuu wa asasi za Kiislamu wamemwandikia barua ya wazi rais mteule wa nchi hiyo Donald Trump na mawaziri wote wa serikali yake kuwataka waheshimu sheria za nchi.

 

Waislamu Marekani wakiandamana kulalamikia chuki dhidi ya Uislamu

Barua hiyo ya Waislamu wa Marekani kwa rais mteule wa nchi hiyo imeandikwa kufuatia ripoti kwamba Trump amepanga kuanzisha mfumo wa uchunguzi, udhibiti na usajili wa taarifa za Waislamu. 

Vitendo vya utumiaji nguvu dhidi ya Waislamu vimeshtadi nchini Marekani baada ya Donald Trump kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa nchi hiyo. Viongozi wa Waislamu nchini humo wanaitakidi kuwa kauli zilizokuwa zikitolewa na Trump katika kipindi cha kampeni za uchaguzi ndizo zilizosababisha kuongezeka hisia za chuki dhidi ya Uislamu.

Trump akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi

Itakumbukwa kuwa miongoni mwa ahadi ambazo Donald Trump aliahidi kuzitekeleza baada ya kushinda uchaguzi wa rais ni kuzuia wahajiri Waislamu kuingia nchini Marekani.../